Uchambuzi wa matini: matumizi ya lugha ya kiswahili katika vivutio vya watalii

dc.contributor.advisorKing'ei, Kitula Osore, Miriam
dc.contributor.authorOnyango, Everline Atieno
dc.date.accessioned2016-08-05T09:45:40Z
dc.date.available2016-08-05T09:45:40Z
dc.date.issued2016
dc.descriptionTasnifu hii imetolewa ili kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Kenyattaen_US
dc.description.abstractUtafiti huu umehusika na uchambuzi wa matini kwa kuangalia matumizi ya lugha katika vivutio vya watalii. Utafiti huu ulichambua matini kwa kuzingatia muktadha wa mawasiliano na hivyo ulijikita katika matini za kimazungurnzo. Katika vivutio vya watalii, wahudumu na watalii walitumia lugha katika mawasiliano yao. Utafiti huu umechanganua lugha katika mawasiliano baina ya wahudumu katika vivutio vya watalii na watalii. Kwa hivyo, malengo ya utafiti huu yalijikita katika kuchanganua sifa bainifu za lugha katika vivutio vya watalii, kubainisha athari za matumizi ya lugha katika vivutio vya watalii kwa wasikizi na msimbo uliotumika katika vivutio vya watalii. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya kidokezi maana fiche cha mazungurnzo iliyoasisiwa na Grice (1975) ambayo inatazama matini kwa narnna ambavyo inakidhi mahitaji ya umilisi wa mawasiliano na utoshelevu wa kipragmatiki. Nadharia ya kidokezi maana fiche cha mazungurnzo ilitumiwa kulingana na malengo ya utafiti huu. Utafiti huu umekuwa wa maktabani na nyanjani. Mtafiti alisoma maandiko kuhusu uchambuzi wa matini kisha mtafiti alielekea nyanjani na alitumia mbinu ya uchunzaji ambapo alisikiliza mawasiliano baina ya wahudumu katika vivutio vya watalii na watalii. Data za utafiti huu zilirekodiwa kwa kutumia vinasa sauti. Utafiti ulionyesha kuwa vivutio vya watalii vina msimbo wake, yaani wahudumu na watalii huzua narnna mbalimbali za kuwasiliana ili kupitisha ujumbe kwa njia ya kipekee. Kuchanganya msimbo kulijitokeza mara tatu katika sentensi kama mwazoni mwa sentensi, katikati ya sentensi na mwishoni mwa sentensi. Vile vile kuchanganya msimbo kulitekeleza majukumufulani katika mawasiliano kama kusisitiza jambo fulani, kurejelea na kufafanua. Ilibainika kuwa katika vivutio vya watalii huwa na sifa za aina mbalimbali kama matumizi ya maswali, utohozi, ufafanuzi, takriri na matumizi ya viziada lugha. Aidha, kulikuwa na athari ya matumizi ya lugha kwa wasikizi katika vivutio vya watalii. Athari hizi zilikuwa mbili, nazo ni athari chanya na athari hasi.Utafiti huu ulikuwa wa muhimu kwa sababu ulituonyesha sifa bainifu za lugha katika vivutio vya watalii na hivyo basi kutambua jinsi wahudumu walivyoweza kuwafanya watalii wengi kuzuru nchini kwa kutumia lugha.en_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/14867
dc.language.isootheren_US
dc.publisherKenyatta Universityen_US
dc.titleUchambuzi wa matini: matumizi ya lugha ya kiswahili katika vivutio vya wataliien_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Uchambuzi wa matini matumizi ya lugha ya kiswahili katika.pdf
Size:
56.85 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full text thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: