Sera ya Lugha na Mabadiliko ya Kimaudhui ya Ushairi wa Kiswahili kati ya Miaka 1930 hadi 1960 nchini Tanzania

dc.contributor.authorNjuguna, Helina Wanjiku
dc.contributor.authorKing’ei, Geoffrey Kitula
dc.contributor.authorWafula, Richard Makhanu
dc.date.accessioned2024-07-05T07:46:54Z
dc.date.available2024-07-05T07:46:54Z
dc.date.issued2023
dc.descriptionArticleen_US
dc.description.abstractMakala hii inachunguza jinsi sera ya lugha ya kipindi cha ukoloni ilivyochochea mabadiliko ya kimaudhui ya ushairi wa Kiswahili kati ya mwaka 1930 hadi 1960 nchini Tanzania. Kulingana na makala hii hali ni matukio mahsusi yanayoathiri ubunifu wa maudhui ya ushairi. Ili kukuza mjadala wetu, makala hii imezingatia sera ya lugha ya kipindi cha utawala wa Wajerumani na Waingereza. Uchunguzi unazingatia mashairi teule kutoka diwani za watunzi wafuatao: Mathias Mnyampala, “Diwani ya Mnyampala (1965)”, Amri Abedi, “Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri (1954)”, Akilimali Snow-White, “Diwani ya Akilimali (1963)”, Shaaban Robert , “ Koja la Lugha (1969), Pambo la Lugha (1966), Kielezo cha Fasili (1968), na Masomo Yenye Adili (1967)”, na Saadani Kandoro, “Mashairi ya Saadani, (1966)”. Mashairi yaliyoteuliwa yanasomwa na kuhakikiwa ili kubainisha maudhui yaliyomo. Uchanganuzi wa data unaongozwa na mihimili ya Nadharia ya Utegemezi na Nadharia ya Ubidhaaishaji wa Lugha. Katika mashairi teule, inabainishwa namna washairi walivyotetea na kuinua hadhi ya lugha ya Kiswahili kwa kueleza sifa na umuhimu wake katika ushairi wao. Pia, inadhihirishwa jinsi ushairi uliotungwa kwa Kiswahili sanifu ulivyotumiwa kama chombo cha umma cha kujieleza kwa kupigania haki, usawa, na uhuru pamoja na kuwahimiza wananchi wakae kwa amani, udugu na heshima.en_US
dc.identifier.citationWanjiku, N. H., & Makhanu, W. R. (2023). Sera ya Lugha na Mabadiliko ya Kimaudhui ya Ushairi wa Kiswahili kati ya Miaka 1930 hadi 1960 nchini Tanzania. Mwanga wa Lugha, 8(1), 25-36.en_US
dc.identifier.urihttps://journals.mu.ac.ke/index.php/mwl/article/view/301
dc.identifier.urihttps://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/28418
dc.language.isoenen_US
dc.subjectSera ya Lughaen_US
dc.subjectUshairien_US
dc.subjectMabadilikoen_US
dc.subjectUbunifuen_US
dc.subjectMaudhuien_US
dc.subjectUtegemezien_US
dc.subjectUbidhaaishajien_US
dc.titleSera ya Lugha na Mabadiliko ya Kimaudhui ya Ushairi wa Kiswahili kati ya Miaka 1930 hadi 1960 nchini Tanzaniaen_US
dc.typeArticleen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Sera ya Lugha na Mabadiliko ya Kimaudhui ya Ushair.pdf
Size:
284.88 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Fulltext article
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: