Matumizi ya jazanda katika tamthilia tatu za Timothy Arege

dc.contributor.advisorWafula, Richard
dc.contributor.advisorMugambi, Peter
dc.contributor.authorOkwena, Sophie
dc.date.accessioned2017-01-12T09:33:04Z
dc.date.available2017-01-12T09:33:04Z
dc.date.issued2013
dc.descriptionTasnifu hii imetolewa u,i kutosheleza mahitaji ya shahada ya uzamili (M.A) katika Chuo Kikuu Cha Kenyatta 2013en_US
dc.description.abstractUtafiti huu umeshughulikia matumizi ya jazanda katika tamthilia za Chamchela ( 2007) , Mstahikiki Meya (2009) na Kijiba cha Mayo (2009) ambazo zimeandikwa na Timothy Arege. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya kimtindo. Nadharia hii ilifaa utafiti huu hasa ikizingatiwa kwamba tamthilia hizi ambazo zimetafitiwa zimesheheni matumizi ya jazanda . Tasnifu hii ina sura sita. Sura ya kwanza imetupa mwelekeo wa utafiti wetu. Hapa tumejadili swala la utafiti, malengo ya utafiti na sababu za kuchagua mada. Hali kadhalika, sura hii imeshughulikia misingi ya nadharia, upeo na mipaka na yaliyoandikwa kuhusu mada. Mwisho ni mbinu za utafiti na uchanganuzi wa data. Sura ya pili inahusika na habari za mtunzi wa tamthilia tatu teule. Katika sura hii tumebainisha historia ya mwandishi ambapo wasifu wa mtunzi na masomo yake yamefafanuliwa. Aidha, mchango wake katika ulingo wa fasihi, waandishi wahornwathiri yote yamefafanuliwa dhahiri. Hatimaye, lugha yake, tajriba yake, utamaduni wake pamoja na muktadha wa lugha yake vimeshughulikiwa. Sura ya tatu imejadili maturnizi ya jazanda katika tamthilia ya Chamchela. Hapa turnejaribu kubainisha aina mbalimbali za jazanda ambazo mtunzi alitumia katika tamthilia hii. Aidha tumeonyesha namna mazingira ya mtunzi na lugha ya mtunzi yamechangia katika uteuzi wake wajazanda. Sura ya nne imechunguza matumizi ya jazanda katika tamthilia ya Mstahiki Meya. Hapa aina mbalimbali za jazanda ambazo mtunzi ametumia zimechunguzwa.Vivyo hivyo, mtunzi ameonyesha jinsi lugha na mazingira yake yalivyochangia katika maturnizi yake ya jazanda. Sura ya tano imejihusisha na matumizi ya jazanda katika tamthilia ya Kijiba cha Mayo. Utafiti umedhihirisha jinsi mwandishi ametumia jazanda za aina mbalimbali katika kuwasilisha ujumbe wake. Aidha, katika sura hii tumebainisha wazi namna lugha na mazingira ya mtunzi yalivyochangia pakubwa katika uteuzi wake wa jazanda. Sura ya sita ni muhtasari wa utafiti, mchango wa utafiti huu, changamoto za utafiti na hatimaye mapendekezo ya utafiti. Utafiti huu ni miongoni mwa tafiti chache ambazo zimewahi kuhakiki tamthilia za Chamchela, Mstahiki Meya na Kijiba cha Mayo kwa kutumia nadharia ya kimtindo. Utafiti huu utawasaidia wahadhiri na wanafunzi wa vyuo vikuu katika kuhakiki kazi zao. Hali kadhalika, utafiti huu utawasaidia walimu na wanafunzi wa shule za sekondari hususan kwa vile tamthilia ya Mstahiki Meya imeteuliwa kutahiniwa. Pia tunaamini kwamba utafiti huu utawasaidia wapenzi wote wa lugha ya Kiswahili.en_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/15275
dc.language.isoKiswahilien_US
dc.publisherKenyatta Universityen_US
dc.titleMatumizi ya jazanda katika tamthilia tatu za Timothy Aregeen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
matumizi ya jazanda katika tamthilia.pdf
Size:
93.62 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full text thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: