Matumizi ya jazanda katika tamthilia tatu za Timothy Arege
Loading...
Date
2013
Authors
Okwena, Sophie
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia matumizi ya jazanda katika tamthilia za Chamchela (
2007) , Mstahikiki Meya (2009) na Kijiba cha Mayo (2009) ambazo zimeandikwa na
Timothy Arege. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya kimtindo. Nadharia hii
ilifaa utafiti huu hasa ikizingatiwa kwamba tamthilia hizi ambazo zimetafitiwa
zimesheheni matumizi ya jazanda .
Tasnifu hii ina sura sita. Sura ya kwanza imetupa mwelekeo wa utafiti wetu. Hapa
tumejadili swala la utafiti, malengo ya utafiti na sababu za kuchagua mada. Hali
kadhalika, sura hii imeshughulikia misingi ya nadharia, upeo na mipaka na
yaliyoandikwa kuhusu mada. Mwisho ni mbinu za utafiti na uchanganuzi wa data.
Sura ya pili inahusika na habari za mtunzi wa tamthilia tatu teule. Katika sura hii
tumebainisha historia ya mwandishi ambapo wasifu wa mtunzi na masomo yake
yamefafanuliwa. Aidha, mchango wake katika ulingo wa fasihi, waandishi
wahornwathiri yote yamefafanuliwa dhahiri. Hatimaye, lugha yake, tajriba yake,
utamaduni wake pamoja na muktadha wa lugha yake vimeshughulikiwa.
Sura ya tatu imejadili maturnizi ya jazanda katika tamthilia ya Chamchela. Hapa
turnejaribu kubainisha aina mbalimbali za jazanda ambazo mtunzi alitumia katika
tamthilia hii. Aidha tumeonyesha namna mazingira ya mtunzi na lugha ya mtunzi
yamechangia katika uteuzi wake wajazanda.
Sura ya nne imechunguza matumizi ya jazanda katika tamthilia ya Mstahiki Meya.
Hapa aina mbalimbali za jazanda ambazo mtunzi ametumia zimechunguzwa.Vivyo
hivyo, mtunzi ameonyesha jinsi lugha na mazingira yake yalivyochangia katika
maturnizi yake ya jazanda.
Sura ya tano imejihusisha na matumizi ya jazanda katika tamthilia ya Kijiba cha
Mayo. Utafiti umedhihirisha jinsi mwandishi ametumia jazanda za aina mbalimbali
katika kuwasilisha ujumbe wake. Aidha, katika sura hii tumebainisha wazi namna
lugha na mazingira ya mtunzi yalivyochangia pakubwa katika uteuzi wake wa
jazanda.
Sura ya sita ni muhtasari wa utafiti, mchango wa utafiti huu, changamoto za utafiti
na hatimaye mapendekezo ya utafiti.
Utafiti huu ni miongoni mwa tafiti chache ambazo zimewahi kuhakiki tamthilia za
Chamchela, Mstahiki Meya na Kijiba cha Mayo kwa kutumia nadharia ya kimtindo.
Utafiti huu utawasaidia wahadhiri na wanafunzi wa vyuo vikuu katika kuhakiki kazi
zao. Hali kadhalika, utafiti huu utawasaidia walimu na wanafunzi wa shule za
sekondari hususan kwa vile tamthilia ya Mstahiki Meya imeteuliwa kutahiniwa. Pia
tunaamini kwamba utafiti huu utawasaidia wapenzi wote wa lugha ya Kiswahili.
Description
Tasnifu hii imetolewa u,i kutosheleza mahitaji ya shahada ya uzamili (M.A) katika Chuo Kikuu Cha Kenyatta 2013