Mtindo wa nyimbo za watoto wa shule za chekechea
Loading...
Date
2015-02-10
Authors
Mwanza, Pius M.
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Tasnifu hii inajadili swala la mtindo wa nyimbo za watoto wa shuJe za chekechea. Nyirnbo kumi na tano za lugha ya Kikamba, pamoja na za KiswahiJi, ziliteuliwa kutoka shule tano za chekechea. Nadharia iliyotumika ni ya uhakiki wa kimtindo ambayo imehusishwa kwa kiasi kikubwa na Coombes H. Mihimili ya nadharia hiyo ilitumika kama dira ya kuuongoza utafiti huu katika kuyafikia malengo yake. Malengo ya utafiti huu yalikuwa ni pamoja na kuvitambua vipengele vya mtindo vilivyotumika katika nyimbo za
watoto wa shule za chekechea na kuonyesha jmsi vilivyochangia katika uwasilishaji wa maudhui. Data iliyotumika katika utafiti huu ilikusanywa maktabani na nyanjani. Maktabani tulipitia vitabu, magazeti, majarida na tasnifu yaliyosaidia kuupa msingi utafiti huu, kinadharia na kimpangilio wa data. Nyanjani tulitumia mbinu ya mahojiano. Data iJiyopatikana, ambayo ilikuwa ni pamoja na nyimbo, ilichanganuliwa kwa kusikilizwa, kunukuliwa na kufasiriwa. Vifaa tulivyotumia katika ukusanyaji data vilikuwa ni pamoja na kinasa sauti, hojaji, karatasi na kalamu. Tulitoa matokeo kupitia njia ya maelezo. Jedwali pia ilitumika kuongezea nguvu maelezo. Matokeo ya uchanganuzi wa data yalidhihirisha kwamba nyimbo .hizi zaweza kutumiwa kufunzia lugha na maudhui kama ilivyo katika tanzu zingine za kifasihi. Mwisho, mapendekezo ya utafiti yalitolewa.
Description
Masters in Education-Department of Kiswahili and African Languages,118p. 2007.