Dini kama chombo cha kuwadhulumu waumini: mifano kutoka fasihi katika kiswahili

dc.contributor.advisorKing'ei, Kitula Osore, Miriam
dc.contributor.authorNg'etich, Kiprugut Daniel
dc.date.accessioned2019-06-19T08:44:05Z
dc.date.available2019-06-19T08:44:05Z
dc.date.issued2011-05
dc.descriptionTasnifu hii imewasillshwa katika idara ya kiswahill na lugha za kiafrika ili kutosheleza baadhi ya mahitaji ya Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta.en_US
dc.description.abstractUtafiti huu umeshughulikia dini kama chombo cha kuwadhulumu waumini katika fasihi andishi ya Kiswahili. Vitabu vilivyoteuliwa na kutumiwa katika utafiti ni : Nitaolewa Nikipenda (1982), Masaibu ya Ndugu Jero (1974), Nguvu ya Sala (1999) na Paradiso (2005). Katika sura ya kwanza ya utafiti tumetanguliza utafiti huku tukijadili mambo yafuatayo kwa kina: utangulizi, swala la utafiti, maswali ya utafiti, madhumuni ya utafiti, sababu ya kuchagua mada, misingi ya nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada, mbinu za utafiti, upeo na mipaka ya utafiti na mbinu za utafiti. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya udenguzi na nadharia ya maadili. Sura ya pili imeweka wazi namna ambavyo dini inadenguliwa kuwa chombo cha dhuluma katika tamthilia ya Nitaolewa Nikipenda na Masaibu ya Ndugu Jero. Katika sura ya tatu tumeeleza jinsi dini inadenguliwa kuwa chombo cha udhalimu katika riwaya ya Paradiso na Nguvu ya Sala. Katika sura ya nne tumefafanua aina za dhuluma za kidini na visababishi vyake. Sura ya tano nayo imejadili athari za dhuluma na jinsi waandishi wa fasihi wametumia mbinu za kisanaa kuunga au kupinga udhalimu wa kidini. Tumehitimisha utafiti wetu na kutoa mapendekezo kwa tafiti zijazo katika sura ya sita. Data za utafiti zimekusanywa, kuchanganuliwa na kuwasilishwa kwa kuzingatia malengo ya utafiti na nadharia teule. Uwasilishaji wa data umefanywa kwa njia ya kimaelezo. Utafiti huu ulimulika kwa undani udhalimu wa kidini. Tulionyesha kuwa dini ni asasi muhimu sana katika jamii. Asasi hii muhimu inaweza kutumiwa kukuza maadili na umoja wa kijamii. Hata hivyo, baadhi ya waumini wametumia nafasi hii kuwadhulumu wenzao. Tulionyesha kuwa ni rahisi kutumia dini kama chombo cha udhalimu kwa sababu aghalabu binadamu hukwepa kupinga chochote kinachohusiana na Mungu au miungu. Nadharia ya udenguzi ilitusaidia kufafanua unafiki wa viongozi wa kidini na nadharia ya maadili ilitufaa katika kujadili dhima ya dini miongoni mwa wanajamii.en_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/19495
dc.language.isoenen_US
dc.publisherKenyatta Universityen_US
dc.titleDini kama chombo cha kuwadhulumu waumini: mifano kutoka fasihi katika kiswahilien_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Dini kama chombo cha kuwadhulumu wauini....pdf
Size:
101.48 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full Text Thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: