Taathira ya dhamira kwa mtindo katika hadithi fupi teule za Kiswahili

dc.contributor.advisorKing'ei, Kitula Osore, Miriam
dc.contributor.authorNtiba, Onesmus Gitonga
dc.date.accessioned2016-11-25T10:20:23Z
dc.date.available2016-11-25T10:20:23Z
dc.date.issued2011-04
dc.descriptionTasnifu hii imewasilishwa katika idara ya kiswahili na lugha za kiafrika va Chuo Kikuu Cha Kenyatta ili kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili. Aprili 2011, PL 8704 .N78T3en_US
dc.description.abstractKatika tasnifu hii tumechunguza athari ya dhamira katika uteuzi wa mtindo katika hadithi fupi teule za Kiswahili. Tumetumia diwani one za mwaka wa 2007. Diwani hizo ni Damu Nyeusi no Hadithi Nyingine (2007), Likizo ya Mauti no Hadithi Nyingine (2007), Kurudi Nyumbani no Hadithi Nyingine (2007) na Alidhani Kapata no Hadithi Nyingine (2007). Malengo ya tasnifu hii yalikuwa ni kuainisha maswala wanayoshughulikia waandishi wa hadithi fupi za 2007 katika diwani zao, kudhihirisha dhamira katika hizo hadithi, kubainisha ni vipi dhamira hizo zinavyouathiri uteuzi wa mitindo wanayoituIDia kuziwasilisha na mwisho kuangazia jinsi mazingira huathiri utunzi wao. Katika utafiti huu, tuliongozwa na Nadharia Changamano inayofumbata baadhi ya mihimili kutoka Nadharia ya Uchanganuzi Saikolojia na Nadharia ya Mtindo. IIi kuipata data faafu, tulitumia mbinu kusudio. Hii ni kwa sababu huu ni utafiti wa kifasihi unaoziJenga diwani teule. Kutokana na utafiti huu, tumelipinga wazo kwamba mwandishi wa hadith fupi hana wakati wa kutosha na hivyo basi anatumia ubanaji unaoathiri dhamira yake. KuJingana na utafiti huu, i1iibuka kuwa mwandishi ana wakati wa kutosha; ni kuamua tu ameamua kuwasilisha dhamira yake kupitia utanzu wa hadithi fupi. Dhamira ya mwandishi huibua uteuzi wa mtindo unaomwezesha kuiwasilisha dhamira yake kikamilifu. Pia ilibainika kuwa maswala wanayoshugbulikia waandishi wa hadithi fupi ni mambo yanayoiathiri jamii ya kisasa. Sura ya kwanza ambayo ni utangulizi imeshughulikia maswala ya kikaida kwa mujibu wa matakwa y~ Idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika, Chuo Kikuu cha Kenyatta kama vile swala la utafiti, sababu za kuchagua mada, malengo ya utafiti, misingi ya nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada hii na mbinu za utafiti. Katika sura ya pili, chimbuko na maendeleo ya utanzu huu wa hadithi fupi yameangaziwa. Pia fasili, muundo na sifa zake utanzu huu zimeangaliwa. Katika sura ya tatu, tumeanza kwa kuyashughulikia mazingira ya waandishi wa hadithi tunazochunguza katika utafiti we.tu . Pia, tumeshughulikia dhamira za dawa za kulevya, ukiukaj i wa haki za mtoto na swala la Ukimwi. Haya tumeyashughulikia kupitia hadithi nane. Sura ya one nayo imeangalia dhamira za kutowajibika kwa viongozi wa kisiasa, migogoro katika ndoa na tamaa ya pesa. Hapa, dhamira hizi zimeangaliwa katika jumla ya hadithi mahsusi kenda. Namna dhamira hizi zinavyoathiri uteuzi wa mitindo imechunguzwa katika sura hizi mbili. Sura ya tano ambayo ni ya mwisho ni hitimisho na matokeo ya utafiti kwa jumla. Pia, imetoa mapendekezo ya utafiti wa baadaye. Utafiti wetu ulifanikiwa na tuna uhakika kuwa umetoa mchango wake katika upanuaji wa welewa wa utanzu huu ambao kwa ulinganifu ndio una historia fupi zaidi katika fasihi ya Kiswahili.en_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/15184
dc.language.isootheren_US
dc.publisherKenyatta Universityen_US
dc.titleTaathira ya dhamira kwa mtindo katika hadithi fupi teule za Kiswahilien_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Taathira va dhamira kwa mtindo katika hadithi fupi.pdf
Size:
51.4 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full text thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: