Dhima ya lugha teule katika kuwasilisha taswira ya mtoto katika jamii ya abagusii tasnifu

dc.contributor.advisorKing'ei, Kitula Osore, Miriam
dc.contributor.authorOmbaye, Robert Omuga
dc.date.accessioned2018-09-10T12:35:02Z
dc.date.available2018-09-10T12:35:02Z
dc.date.issued2018
dc.descriptionTasnifu hii imetolewa ili kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu Cha Kenyattaen_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulichunguza dhima ya lugha teule katika kuwasilisha taswira ya mtoto katika jamii ya Abagusii. Malengo ya utafiti huu yalikuwa kutambua lugha iliyowasilisha taswira ya mtoto na kubainisha dhima na athari zake katika jamii ya Abagusii. Nadharia ya Ethnografia ya Mawasiliano iliyoasisiwa na Hymes (1964) ilitumika katika utafiti huu. Nadharia hiyo ilifaa kwa sababu iliangazia jinsi mawasiliano yalivyochanganuliwa kwa kuzingatia vipengele vya: mada, umbo la ujumbe, muktadha, wahusika, sababu za mawasiliano, kanuni za ufafanuzi wa ujumbe, njia za mawasiliano na utendaji. Data ya kimsingi ilipatikana kutoka eneo bunge la Nyaribari Chache, Ugatuzi Mdogo wa Kisii ya Kati, Kaunti ya Kisii. Aidha, data nyingine ilikusanywa maktabani kwa kusoma vitabu, kumbukumbu, ripoti, tasnifu, makala na majalida kuhusu mada ya utafiti. Nyanjani mtafiti alitumia sampuli iliyoteuliwa kwa kutumia mbinu ya kimakusudi kuwahoji watu sabini na wawili. Mbinu ya makusudi ilitumiwa kupata watafitiwa walioimudu vyema lugha ya Ekegusii kuhojiwa ili kupata matokeo faafu. Mtafiti aliwahoji watu wawili (2) kutoka kila kikundi; watoto, vijana, watu wazima, naibu wa machifu, machifu na wataalamu wa haki za watoto kutoka wodi sita (6) za eneo bunge la Nyaribari Chache. Vifaa vilivyotumiwa kuwahoji ni hojaji wazi na maswali ya mahojiano ya ana kwa ana na wahojiwa. Data iliyokusanywa ilirekodiwa na kuchanganuliwa kwa kuzingatia maswali, malengo na nadharia ya utafiti. Matokeo ya utafiti huu yaliwasilishwa kwa kutumia maelezo na yalibainisha kuwa, lugha hasi na chanya ilitumika katika kuwasilisha taswira mbalimbali za watoto katika jamii ya Abagusii. Matokeo ya utafiti huu vilevile yalibainisha kuwa dhima za lugha hiyo ni: kuelimisha, kukuza maadili, kuonya, kurekebisha tabia, kuwasiliana, kutia motisha, kusifu, kufariji, kulinganisha, kushauri na kukemea. Aidha, matokeo ya utafiti huu yalibainisha kuwa lugha hiyo ilizua athari kadhaa kwa mtoto ambazo ni: kuhama kutoka nyumbani kwao, kutelekezwa, kubaguliwa, kukata tamaa, kuchanganyikiwa akili, kuwa na tabia nzuri au mbaya, kupendwa, kukubalika na kufurahi. Utafiti huu ulikuwa wa manufaa katika jamii ya Abagusii kwa vile uliwawezesha kuelewa kuhusu lugha iliyowasilisha taswira ya mtoto. Ufahamu wa lugha hiyo ni muhimu kwa vile ulichangia katika kuamua maisha ya mtoto siku za usoni. Aidha, ufahamu huo ulichangia pakubwa katika utoaji wa mielekeo, maoni na matendo ya watu wazima kwa watoto katika jamii ya Abagusii.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/18557
dc.language.isootheren_US
dc.publisherKenyatta Universityen_US
dc.titleDhima ya lugha teule katika kuwasilisha taswira ya mtoto katika jamii ya abagusii tasnifuen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Dhima ya lugha teule katika kuwasilisha taswira ya mtoto....pdf
Size:
930.98 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full text thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: