Ukiukaji wa Kanuni Bia za Greenberg katika Miundo ya Tungo Zenye Vihusishi Katika Lugha ya Kiswahili
dc.contributor.author | Ongwae, Jemimah Kwamboka | |
dc.contributor.author | Githinji, Peter | |
dc.date.accessioned | 2024-10-03T09:05:50Z | |
dc.date.available | 2024-10-03T09:05:50Z | |
dc.date.issued | 2023-11 | |
dc.description | Article | |
dc.description.abstract | Makala haya yalidhamiria kubaini ukiukaji wa baadhi ya kanuni bia za Greenberg katika miundo ya tungo zenye vihusishi vya Kiswahili. Katika utafiti wake, Greenberg (1963), alipendekeza kanuni bia 45 na kutafiti lugha 30 ili kuchunguza mpangilio wa vipashio vya kiisimu katika makundi mbalimbali ya lugha. Lugha ya Kiswahili ilikuwepo mojawapo ya sampuli alizoteua. Hata hivyo, katika kuzingatia uwekaji vihusishi, inaonekana kukiuka baadhi ya kanuni hizo. Kwa hivyo, mkabala wa Greenberg (1963) ulitumika. Kanuni bia za Greenberg hasa zile zinazozungumzia vihusishi pekee zilitumika kuchanganua miundo na mazingira ya kiisimu yanayosababisha ukiukaji wa baadhi ya kanuni za Greenberg katika uwekaji wa vihusishi vya Kiswahili. Data iliyotumika ilikuwa ni tungo zenye vihusishi. Mbinu ya usampulishaji wa kimakusudi ilitumika kuteua vihusishi hivi na vilikusanywa kwa kusoma vitabu vya sarufi na makala kutoka kwenye majarida na makala ya mtandaoni. Data ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa kuzingatia mkabala wa kanuni bia za Greenberg kupitia ufafanuzi wa data kwa njia ya maelezo na unukuzi wa kanuni bia za Greenberg. Ilijidhihirisha kuwa baadhi ya kanuni bia za Greenberg zina ukiushi katika lugha ya Kiswahili. Ukiushi hasa ulitokea kwa sababu sifa A haikumiliki sifa B kwa kuzingatia sheria ya uchanganuzi iliyopeanwa. Haya yalibainika hasa kwa kuwa lugha ya Kiswahili inamiliki aina mbili za vihusishi; vihusishi vya kabla ya nomino na vihusishi vya baada ya nomino katika umbo lake la nje. Hata hivyo, baadhi ya kanuni bia zingine zilionyesha utiifu. Aidha baadhi ya kanuni hizi zina utata ambao unaleta changamoto katika juhudi za kutoa kauli jumlishi. Makala haya yatachangia katika kongoo ya utaratibu wa vipashio katika sentensi, taipolojia ya lugha na sintaksia ya Kiswahili. | |
dc.identifier.citation | Ongwae, J. K. & Githinji, P. (2023). Ukiukaji wa Kanuni Bia za Greenberg katika Miundo ya Tungo Zenye Vihusishi Katika Lugha ya Kiswahili. East African Journal of Swahili Studies, 6(2), 30-43. https://doi.org/10.37284/jammk.6.2.1596. | |
dc.identifier.uri | https://doi.org/10.37284/jammk.6.2.1596 | |
dc.identifier.uri | https://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/29046 | |
dc.language.iso | other | |
dc.publisher | EANSO | |
dc.title | Ukiukaji wa Kanuni Bia za Greenberg katika Miundo ya Tungo Zenye Vihusishi Katika Lugha ya Kiswahili | |
dc.type | Article |