Tathmini ya Mtalaa wa Isimu Jamii wa Shule za Upili Nchini Kenya

dc.contributor.advisorKing'ei, Kitula Osore, Miriam
dc.contributor.authorNgugi, Mwangi Boniface
dc.date.accessioned2016-03-30T09:03:05Z
dc.date.available2016-03-30T09:03:05Z
dc.date.issued2008
dc.descriptionTasnifu Hii Imewasilishwa katika Idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika ili Kutosheleza Baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, 2008en_US
dc.description.abstractUtafiti huu umeshughulikia kutathmini mtalaa wa Isimujamii wa shule za upili nchini Kenya. Utafiti huu ulidhamiria kutathrriini na kuimarisha mtalaa wa Isimujamii katika lugha ya Kiswahili kama chombo cha mawasiliano kwa kuongozwa na misingi ya nadharia za ufundishaji wa Lugha ya Pili na Isimujamii. Utafiti huu pia ulibainisha changamoto zinazowakumba walimu wanapofundisha Isimujamii iliyojumuishwa katika silabasi ya mtalaa wa sasa. Wilaya ya Thika ilichaguliwa kama eneo la utafiti kwa vile ina shule za Taifa, Mkoa, Wilaya na za Kibinafsi zilizohitajika kufanyia utafiti. Ukusanyaji wa data ulifanywa kupitia mahojiano ya walimu, watalaamu wa elimu na kuchunguza ratiba ya vipindi vya masomo kutoka kidato cha kwanza hadi cha nne. Dhana ya mitalaa pamoja na uandalizi wa mitalaa imepitiwa kwa vile ni muhimu katika utekelezaji wa mtalaa wowote mpya. Maoni ya walimu na wakuza mitalaa kuhusu dhana ya mtalaa na maandalizi yake yamewasilishwa kwa njia ya mjadala. Vile vile, uchanganuzi wa maoni ya walimu na wakuza mitalaa kuhusu mawanda ya Isimujamii umeshughulikiwa. Hatimaye matokeo ya utafiti huu pamoja na mapendekezo yameshughulikiwa ambapo imebainika kuwa, mtalaa wa Isimujamii una udhaifu katika kumwongoza mwalimu ili aimarishe kiwango cha mawasiliano cha wanafunzi. Walimu wengi wanasisitiza miundo ya lugha badala ya uamilifu wa lugha. Jambo jingine linalotinga utekelezaji wa mtalaa wa Isimujamii ni ukosefu wa vifaa vya kufundishia. Utafiti huu utafaidi sera na upangaji wa lugha. IIi kuimarisha uhusiano mwema katika jamii yenye lugha nyingi, lugha moja inahitajika. Lugha kama hiyo itapatikana kwa kuifunza shuleni.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/14520
dc.language.isoenen_US
dc.publisherKenyatta Universityen_US
dc.titleTathmini ya Mtalaa wa Isimu Jamii wa Shule za Upili Nchini Kenyaen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Tathmini ya Mtalaa wa Isimujamii......pdf
Size:
65.26 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full Text Thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: