Matumizi ya lugha katika sherehe za kumfunda mwali (dhifa za jikoni) miongoni mwa wazaramo

dc.contributor.advisorMomanyi, Clara
dc.contributor.advisorMwita, Chacha
dc.contributor.authorMosha, Felician Doroth
dc.date.accessioned2011-11-02T08:39:06Z
dc.date.available2011-11-02T08:39:06Z
dc.date.issued2011-11-02
dc.descriptionPL 8702 .M63
dc.description.abstractDhifa za jikoni ni sherehe zinazoadhimishwa katika makabila mengi nchini Tanzania. Sherehe hizi hutofautiana kwa kiasi fulani kulingana na kabila husika. Hii ni kwa sababu kila kabila lina utamaduni unaojibainisha na kabila jingine. Utafiti huu unahusu uchunguzi wa dhifa za jikoni katika jamii ya Wazaramo. Utafiti umehakiki matumizi ya tamathali za usemi. Tamathali mbili; tashibihi na sitiari ndizo zilizozingatiwa kwa kuwa zina nafasi kubwa katika sherehe hizo. Katika kufanikisha malengo ya utafiti, nadharia ya Ethnografia ya Mawasiliano imetumika katika uchanganuzi wa data. Data ilikusanywa kutoka mkoa wa Dar es Salaam katika mtaa wa Magomeni, nchini Tanzania. Mbinu ya kushiriki katika sherehe hizo ilitumika katika zoezi la kukusanya data, sanjari na matumizi ya hojaji na kanda zilizorekodiwa. Uchunguzi umedhihirisha kuwa matumizi ya tamathali hizo hubeba ujumbe mzito kwa mwali na kundi-jamii kwa jumla. Humsaidia mwali na hadhira kuupata vizuri ujumbe uliokusudiwa kwa njia fupi na kuufanya unate vizuri akilini na kuuhusisha na uhalisi wa kila siku wa maisha ya jamii. Pia husaidia hadhira kuendelea kuwa na motisha wa kusikiliza kinachowasilishwa. Vilevile imebainika kuwa wawasilishaji wa mawaidha wana mbinu bunifu za kuunda tashibihi na sitiari, huku wakizingatia vipengele vichache 'vya kitamaduni. Tamathali hizi zimeonekana kuwa na miundo ya wazi, kijazanda na kimethali. Swala la muktadha ndilo linalotawala mawasiliano katika Dhifa za jikoni na hivyo kuimarisha mawasiliano kati ya kundi-jamii hilo. Pia imegundulika kuwa baadhi ya vifaa vya upambaji na zawadi anazopewa mwali si katika matumizi ya kawaida tu, bali huashiria dhana fulani kimuktadha. Dhifa za jikoni ni uwanda ambao unahitaji tafiti zaidi za kitaaluma kutokana na majukumu yake kwa jamii. Inapendekezwa kuwa tafiti zifanywe katika vipengele vingine vya lugha na maudhui. Aidha, tafiti linganishi zifanywe kwa jamii zenye sherehe hizi. Kadhalika, Wazaramo wana sherehe za unyago na dhifa za jikoni. Hivyo, utafiti linganishi unahitajika katika sherehe hizi mbili.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/1529
dc.language.isootheren_US
dc.titleMatumizi ya lugha katika sherehe za kumfunda mwali (dhifa za jikoni) miongoni mwa wazaramoen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Matumizi ya lugha katika sherehe za kumfunda mwali.pdf
Size:
74.05 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full text thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: