Matumizi ya lugha katika sherehe za kumfunda mwali (dhifa za jikoni) miongoni mwa wazaramo

Loading...
Thumbnail Image
Date
2011-11-02
Authors
Mosha, Felician Doroth
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Dhifa za jikoni ni sherehe zinazoadhimishwa katika makabila mengi nchini Tanzania. Sherehe hizi hutofautiana kwa kiasi fulani kulingana na kabila husika. Hii ni kwa sababu kila kabila lina utamaduni unaojibainisha na kabila jingine. Utafiti huu unahusu uchunguzi wa dhifa za jikoni katika jamii ya Wazaramo. Utafiti umehakiki matumizi ya tamathali za usemi. Tamathali mbili; tashibihi na sitiari ndizo zilizozingatiwa kwa kuwa zina nafasi kubwa katika sherehe hizo. Katika kufanikisha malengo ya utafiti, nadharia ya Ethnografia ya Mawasiliano imetumika katika uchanganuzi wa data. Data ilikusanywa kutoka mkoa wa Dar es Salaam katika mtaa wa Magomeni, nchini Tanzania. Mbinu ya kushiriki katika sherehe hizo ilitumika katika zoezi la kukusanya data, sanjari na matumizi ya hojaji na kanda zilizorekodiwa. Uchunguzi umedhihirisha kuwa matumizi ya tamathali hizo hubeba ujumbe mzito kwa mwali na kundi-jamii kwa jumla. Humsaidia mwali na hadhira kuupata vizuri ujumbe uliokusudiwa kwa njia fupi na kuufanya unate vizuri akilini na kuuhusisha na uhalisi wa kila siku wa maisha ya jamii. Pia husaidia hadhira kuendelea kuwa na motisha wa kusikiliza kinachowasilishwa. Vilevile imebainika kuwa wawasilishaji wa mawaidha wana mbinu bunifu za kuunda tashibihi na sitiari, huku wakizingatia vipengele vichache 'vya kitamaduni. Tamathali hizi zimeonekana kuwa na miundo ya wazi, kijazanda na kimethali. Swala la muktadha ndilo linalotawala mawasiliano katika Dhifa za jikoni na hivyo kuimarisha mawasiliano kati ya kundi-jamii hilo. Pia imegundulika kuwa baadhi ya vifaa vya upambaji na zawadi anazopewa mwali si katika matumizi ya kawaida tu, bali huashiria dhana fulani kimuktadha. Dhifa za jikoni ni uwanda ambao unahitaji tafiti zaidi za kitaaluma kutokana na majukumu yake kwa jamii. Inapendekezwa kuwa tafiti zifanywe katika vipengele vingine vya lugha na maudhui. Aidha, tafiti linganishi zifanywe kwa jamii zenye sherehe hizi. Kadhalika, Wazaramo wana sherehe za unyago na dhifa za jikoni. Hivyo, utafiti linganishi unahitajika katika sherehe hizi mbili.
Description
PL 8702 .M63
Keywords
Citation