Uchanganuzi wa usemi katika sajili ya dini: sifa bainifu za lugha ya mahubiri

dc.contributor.advisorKing'ei, Kitula Osore, Miriam
dc.date.accessioned2016-07-18T11:57:36Z
dc.date.available2016-07-18T11:57:36Z
dc.date.issued2001
dc.descriptionIdara ya kiswaillli na lugha za kiafrika Chuo Kikuu cha Kenyatta tasnifu hii imetolewa ili kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili (Master of Arts) katika Chuo Kikuu cha Kenyatta. 2001en_US
dc.description.abstractKatika tasnifu hii, tumechunguza sifa bainifu za lugha ya mahubiri kama zinavyojitokeza katika sajili ya dini katika lugha ya Kiswahili. Tumetumia data kutokana na mahubiri mbalimbali na kuyachanganua ili kudhihirisha sifa zake. Utafiti huu ulikuwa na malengo mawili ambayo ulitekeleza. Kulikuwa na utambuzi wa sifa bainifu za lugha ya mahubiri na utambuzi wa aina za mshikamano na jinsi zinavyounganisha. mahubiri. Katika kufanya hivi, mtazamo wa kimtindo na wa mshikamano katika nadharia ya uamilifu wa lugha ilitumika. Sura ya kwanza ambayo ni utangulizi wa tasnifu imeshughulikia swala la utafiti, sababu za kuchagua swala lenyewe, madhumuni ya utafiti, upeo wa utafiti, misingi ya kinadharia, yaliyoandikwa kuhusu somo lile na mbinu za utafiti. Ni katika sura ya pili ambapo tumejishughulisha na baadhi ya sifa bainifu katika lugha ya mahubiri kama vile jinsi wahubiri wanavyoanza mahubiri yao, njia wanazoturnia kuendeleza ujumbe, na namna wanavyohitimisha. Kutokana na uchunguzi wetu tuligundua ya kwamba kuna mianzo maalum ya kuanza mahubiri. Kwa jumla wahubiri huanza kwa maamkuzi na pia kutaja kiini cha ujumbe wao.Wahubiri hutumia njia nyingi kuendeleza ujumbe kama vile matumizi ya mifano takriri, kubadilisha sauti, maswali na kadhalika. Pia, kuna njia maalum za kutamatisha mahubiri. Katika kila ruwaza iliyojadiliwa, maelezo ya kiisimu yametolewa. Sura ya tatu yaonyesha kuwa mahubiri yana sifa ya kuchanganya msimbo. Kuchanganya msimbo kumeshughulikiwa kama mojawapo ya sifa bainifu katika kuendeleza ujumbe. viii • Aina muhimu za kuchanganya msimbo na JlOS1 zinavyojitokeza katika matini za uchanganuzi zimejadiliwa. Sura ya nne yaonyesha kuwa lugha ya mahubiri ina aina mbalimbali za mshikamano. Kwa mfano, kuna mshikamano wa kimsamiati, urejeshi, uunganishi, ubadilishaji na udondoshi. Sura ya tano na ya mwisho inajumuisha muhstasari na matokeo ya utafiti kwa jumla. Mapendekezo ya utafiti mwingine unaoweza kufanywa katika uwanja huu pia yamewekwa katika sura hiien_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/14837
dc.language.isoenen_US
dc.titleUchanganuzi wa usemi katika sajili ya dini: sifa bainifu za lugha ya mahubirien_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Uchanganuzi wa usemi katika sajili ya dini sifa bainifu za lugha ya mahubiri.pdf
Size:
64.77 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Thesis full text
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: