Mbinu na Mikakati ya Kutumia Fasihi ya Watoto kama Bibliotherapia'

dc.contributor.authorNgugi, Pamela M.Y.
dc.date.accessioned2024-02-09T05:52:46Z
dc.date.available2024-02-09T05:52:46Z
dc.date.issued2015
dc.descriptionArticleen_US
dc.description.abstractKatika ulimwengu wa sasa, sanaa ya uchoraji, dansi, muziki na hata fasihi imechukuliwa kama aina moja ya tiba kwa wagonjwa wanaougua magonjwa mbalimbali. Wataalamu wa tiba-therapia wameanza kutumia fasihi kama njia ya kuwasaidia wanajamii kukabiliana na hali mbalimbali za kijamii baada ya kugundua nafasi muhimu ya vitabu katika kutibu wagonjwa na wanajamii wengine wanaopitia hali ngumu za kijamii. Fasihi ya watoto kama ilivyo fasihi ya watu wazima ina majukumu mbalimbali katika jamii yoyote ya binadamu. Kupitia fasihi, wanajamii hujuzwa, huelimishwa na kuburudishwa. Fasihi ya watoto huwa na lengo maalum katika maisha ya watoto kwani inaweza kutumika kama kitulizo cha moyo kutokana na hali mbalimbali zinazowakumba watoto wa kisasa. Hadithi za watoto zinaweza kutumika kama njia mbadala za namna ya kukabiliana na hali ngumu za kimaisha. Usomaji wa vitabu vya fasihi ya watoto unaweza kutumika kama kichocheo cha mijadala ama darasani au hata nyumbani kuhusiana na hali mbalimbali zinazowakumba watoto katika viwango mbalimbali vya ukuaji. Lengo la makala hii ni kubainisha mbinu na mikakati ya kutumia fasihi ya watoto kama bibliotherapia. Katika kutekeleza hili, makala itaeleza dhana ya bibliotherapia pamoja na kubainisha njia mwafaka zinazoweza kutumiwa na wadau hasa walimu katika kutumia vitabu kama bibliotherapia miongoni mwa wanafunzi wao. Pamoja na hayo, mifano ya narnna bibliotherapia inavyotumika katika hali mbalimbali za watoto imetolewa.en_US
dc.identifier.citationNgugi, P. M. (2017). Mbinu na Mikakati ya Kutumia Fasihi ya Watoto kama Bibliotherapia. Kioo cha Lugha, 13(1).en_US
dc.identifier.urihttps://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/27609
dc.language.isoenen_US
dc.publisherJournals.UDSMen_US
dc.titleMbinu na Mikakati ya Kutumia Fasihi ya Watoto kama Bibliotherapia'en_US
dc.typeArticleen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Mbinu na Mikakati ya Kutumia Fasihi ya Watoto kama Bibliotherapia'.pdf
Size:
7.48 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full text Article
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: