Mbinu na Mikakati ya Kutumia Fasihi ya Watoto kama Bibliotherapia'
Loading...
Date
2015
Authors
Ngugi, Pamela M.Y.
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Journals.UDSM
Abstract
Katika ulimwengu wa sasa, sanaa ya uchoraji, dansi, muziki na hata fasihi imechukuliwa kama aina
moja ya tiba kwa wagonjwa wanaougua magonjwa mbalimbali. Wataalamu wa tiba-therapia
wameanza kutumia fasihi kama njia ya kuwasaidia wanajamii kukabiliana na hali mbalimbali za
kijamii baada ya kugundua nafasi muhimu ya vitabu katika kutibu wagonjwa na wanajamii wengine
wanaopitia hali ngumu za kijamii. Fasihi ya watoto kama ilivyo fasihi ya watu wazima ina
majukumu mbalimbali katika jamii yoyote ya binadamu. Kupitia fasihi, wanajamii hujuzwa,
huelimishwa na kuburudishwa. Fasihi ya watoto huwa na lengo maalum katika maisha ya watoto
kwani inaweza kutumika kama kitulizo cha moyo kutokana na hali mbalimbali zinazowakumba
watoto wa kisasa. Hadithi za watoto zinaweza kutumika kama njia mbadala za namna ya
kukabiliana na hali ngumu za kimaisha. Usomaji wa vitabu vya fasihi ya watoto unaweza kutumika
kama kichocheo cha mijadala ama darasani au hata nyumbani kuhusiana na hali mbalimbali
zinazowakumba watoto katika viwango mbalimbali vya ukuaji. Lengo la makala hii ni kubainisha
mbinu na mikakati ya kutumia fasihi ya watoto kama bibliotherapia. Katika kutekeleza hili, makala
itaeleza dhana ya bibliotherapia pamoja na kubainisha njia mwafaka zinazoweza kutumiwa na
wadau hasa walimu katika kutumia vitabu kama bibliotherapia miongoni mwa wanafunzi wao.
Pamoja na hayo, mifano ya narnna bibliotherapia inavyotumika katika hali mbalimbali za watoto
imetolewa.
Description
Article
Keywords
Citation
Ngugi, P. M. (2017). Mbinu na Mikakati ya Kutumia Fasihi ya Watoto kama Bibliotherapia. Kioo cha Lugha, 13(1).