Athari za Sera ya Lugha Afrika Mashariki na Nafasi ya Kiswahili Afrika na Ulimwenguni

Loading...
Thumbnail Image
Date
2024
Authors
Osore, Miriam
Minyade, Sheril
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
RealText Printers and Publishers
Abstract
Sera ya lugha ni kipengele cha mpango lugha. Haya ni maamuzi katika maandishi kuhusu jinsi lugha zinavyopaswa kutumika katika jamii ili kutekeleza majukumu mbalimbali. Maamuzi haya yanaweza kutolewa katika katiba ya nchi husika. Sera ya lugha Afrika Mashariki imepitia mabadiliko kuanzia enzi za ukoloni hadi sasa. Hata kabla ya ukoloni, Kiswahili kilikuwa tayari kinatumika kama lugha ya mawasiliano mapana katika biashara kati ya Waarabu na Waafrika. Wamishonari waliofika eneo la Afrika Mashariki walikuta Kiswahili kimeenea wakakitumia kueneza dini. Hatua za mwanzo za usanifishaji wa Kiswahili zilichukuliwa na wamishonari walioona haja ya kusanifisha Kiswahili ili kukitumia kwa mafanikio zaidi ya kueneza injili. Kiunguja kiliteuliwa kama msingi wa kusanifisha Kiswahili. Kiswahili sanifu ndicho kilitumiwa katika .maandishi. Wakoloni walipofika katika eneo la Afrika Mashariki pia walianza kukitumia Kiswahili katika shughuli za utawala na elimu. Kila nchi ilikuwa na sera tofauti za lugha: Uganda, chini ya Waingereza haikukipa Kiswahili nafasi ya kuenea. Waingereza waliotawala Kenya walisisitiza matumizi ya Kiingereza na lugha ya kwanza. Tanzania ilitawaliwa na Wajerumani na Waingereza. Kiswahili kilipewa kipaumbele; kilitumika katika shughuli zote za elimu na utawala fakala hii inalenga kubainisha jinsi sera tofauti za lugha katika nchi hiziwakati wa ukoloni na baada ya ukoloni zimeathiri kuenea kwa Kiswahili Afrika na ulimwenguni.
Description
Book Chapter
Keywords
Sera, Mpango wa lugha, Maendeleo ya Kiswahili
Citation