Athari ya mazingira ya kihistoria na kijamii katika uwasilishaji wa maudhui ya dhifa (E. Kezilahabi)

dc.contributor.advisorKing'ei, Kitula Osore, Miriam
dc.contributor.authorNasimiyu, Christine M.
dc.date.accessioned2016-11-23T13:25:43Z
dc.date.available2016-11-23T13:25:43Z
dc.date.issued2016
dc.descriptionTasnifu hii imew asilishw a kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya Uzamili ya Chuo Kikuu Cha Kenyatta, 2016en_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulichunguza athari ya mazingira ya kihistoria na kijamii katika uwasilishaji wa maudhui ya diwani ya Dhifa ya E. Kezilahabi (2008). Malengo yalikuwa, kubainisha maudhui yaliyowasilishwa na mtunzi wa Dhifa, kubainisha narnna maudhui haya yalivyowasilishwa na kueleza narnna maudhui haya yalivyoibua mazingira ya kijamii na kihistoria. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Uhistoria Mpya ambayo huangalia umuhimu wa muktadha katika utunzi na uhakiki wa kazi za kifasihi. Pia, huonyesha ya kwamba kadiri jamii zinavyoendelea, utamaduni hubadilika kiwakati na jambo hili huathiri utunzi, uwasilishaji na uhakiki wa kazi za kifasihi. Utafiti huu ulizingatia muundo wa kimaelezo kuhusu suala la utafiti, msingi wa nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada na mbinu za utafiti. Utafiti huu ulifanywa maktabani. Sampuli iliteuliwa kimakusudi ambapo mashairi ishirini na moja yaliteuliwa ili saba yashughulikie kipengele cha siasa, uchumi na masuala ya kijamii. Data ilikusanywa kutokana na usomaji wa kina wa mashairi teule. Uchanganuzi wa data ulizingatia uainishaji wa aina ya maudhui, uwasilishaji wake pamoja na matukio ya kihistoria. Aidha, ulizingatia chimbuko la maudhui, namna yalivyowasilishwa, dhamira na falsafa ya mtunzi. Hayo yote yalifanywa kwa kuzingatia pengo lililonuiwa kujazwa na utafiti huu kwa kuongozwa na nadharia ya utafiti. Utafiti ulibaini na kutambua kwamba, siasa ya Tanzania, baada ya Azimio la Arusha ilichukuwa rnkondo mpya. Aidha, mazingira mbalimbali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi yalichangia pakubwa katika kuwasilisha maudhui ya diwani ya Dhifa. Inatarajiwa kuwa utafiti huu utawafaa wanafunzi wa shule za upili, vyuo, watafiti wa ushairi na wakuza mitalaa. Tasnifu hii iligawanywa katika sura sita. Sura ya kwanza ilishughulikia mada ya utafiti, maswali ya utafiti, malengo ya utafiti, upeo na mipaka, yaliyoandikwa kuhusu mad a, sababu za kuchagua mada na misingi ya nadharia. Sura ya pili ilichunguza historia na falsafa ya mtunzi. Sura ya tatu iliangazia maudhui ya kisiasa. Sura ya nne ilichambua maudhui ya kiuchumi. Sura ya tano iliangalia maudhui ya kijamii. Sura ya sita ilijumuisha muhtasari, hitimisho,matokeo ya utafiti na mapendekezo.en_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/15175
dc.language.isoKiswahilien_US
dc.publisherKenyatta Universityen_US
dc.titleAthari ya mazingira ya kihistoria na kijamii katika uwasilishaji wa maudhui ya dhifa (E. Kezilahabi)en_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Athari ya mazingira ya kihistoria na kijamii katika.pdf
Size:
59.59 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full text thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: