Dhuluma za Kitabaka katika Riwaya za Mkamandume na Shetani Msalabani

dc.contributor.advisorKitula King‟eien_US
dc.contributor.advisorJaphet M. Mukobwaen_US
dc.contributor.authorKausi, Barasa George
dc.date.accessioned2022-04-08T10:07:57Z
dc.date.available2022-04-08T10:07:57Z
dc.date.issued2021
dc.descriptionTasnifu hii Imetolewa ili Kutosheleza Baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, Novemba, 2021en_US
dc.description.abstractUtafiti huu umebainisha namna masuala ya dhuluma za kitabaka yanavyojitokeza katika riwaya za Mkamandume (2004) na Shetani Msalabani (1982). Waandishi wa riwaya hizi; Said A. Mohamed na Ngugi wa Thiong’o mtawalia wametuchorea picha halisi ya namna dhuluma za kitabaka zimekithiri katika jamii wanamoishi. Katika riwaya teule, wahusika wanyonge kutoka tabaka la chini wamedhulumiwa na wahusika wa tabaka la juu kwa misingi ya kiuchumi. Hali hii imechangia utengano uliopo baina ya wahusika maskini na matajiri katika riwaya za utafiti. Malengo ya utafiti yalikuwa ni kuonyesha jinsi dhuluma za kitabaka zinavyobainika katika riwaya teule, kubainisha athari zake kwa wahusika na kuchunguza mbinu wanazotumia wanyonge kujikomboa na kujiimarisha kimaisha. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Uhakiki wa ki-Marx ambayo iliasisiwa na Karl Marx na Engles (1959). Nadharia hii inaeleza kuwa historia ya maisha ya binadamu inaweza kuelezeka katika misingi yakinifu ya kiuchumi ambayo huchunguza njia kuu za uzalishaji na usambazaji mali. Tabaka la juu lenye watu wachache huwa na uwezo mwingi kiuchumi kuliko tabaka la chini lenye watu wengi wasiomiliki mali. Pia huonyesha namna jamii huimarika kutokana na migogoro ya kitabaka baina ya watu wa tabaka la chini dhidi ya wale wa tabaka la juu. Utafiti huu uligundua kwamba riwaya za Mkamandume na Shetani Msalabani zimeonyesha kwa undani namna tabaka nyonyaji linavyowanyonya wachochole wa tabaka la chini. Riwaya hizi zimebainisha suala la kiuchumi kama chanzo cha dhuluma zinazowakumba wahusika wanyonge. Aidha, dhuluma hizi zimesababisha athari chungu nzima katika tabaka la walalahoi. Vilevile, utafiti huu umebainisha kuwa wanyonge katika riwaya teule wanaungana na kujikomboa kiuchumi, kisiasa na kielimu. Mbinu walizotumia kupigania ukombozi ni: maandamano, migomo kazini, kuelimika kimasomo, uandishi wa vitabu vya fasihi na kuanzisha biashara ili kujikimu kimaisha. Utafiti huu utawazindua wahusika wanyonge kujikomboa dhidi ya dhuluma za kitabaka katika jamii.en_US
dc.description.sponsorshipChuo Kikuu cha Kenyattaen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/23539
dc.language.isootheren_US
dc.publisherKenyatta Universityen_US
dc.subjectDhulumaen_US
dc.subjectKitabakaen_US
dc.subjectRiwayaen_US
dc.subjectMkamandumeen_US
dc.subjectShetani Msalabanien_US
dc.titleDhuluma za Kitabaka katika Riwaya za Mkamandume na Shetani Msalabanien_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Dhuluma za Kitabaka ....pdf
Size:
831.13 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Fultext thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: