Uchunguzi wa uozo katlka mashairi ya Khatib na King'ei

dc.contributor.advisorKing'ei, Kitula Osore, Miriam
dc.contributor.authorBarasa, Ayub O.
dc.date.accessioned2016-02-17T12:02:11Z
dc.date.available2016-02-17T12:02:11Z
dc.date.issued2015-12
dc.descriptionDepartment of Kiswahili and African Languages, 111p. Dec.2015, The PL 8704 .U3B3en_US
dc.description.abstractUtafiti huu umeshughulikia uozo katika mashairi ya Khatib na King'ei kwa kuongozwa na nadharia ya kimtindo na maadili. Nadharia hizi zilifaa utafiti huu ikizingatiwa kwamba maudhui ya mtunzi na mtindo anaoutumia katika kutoa ujumbe wake ni vipengele vinavyotegemeana. Mtunzi hutunga kutokana na tajriba aliyopata katika mazingira yake na lugha ndiyo aitumiayo kueleza mambo mbalimbali ya jamii yake kwa njia ya kubuni. Tasnifu hii ina sura tano. Sura ya kwanza imetupa mwelekeo wa utafiti, malengo ya utafiti na sababu za kuchagua mada. Hali kadhalika sura hii imeshughulikia misingi ya nadharia, upeo na mipaka na yaliyoandikwa kuhusu mada. Mwisho ni mbinu za utafiti na uchanganuzi wa data. Sura ya pili imejadili mashairi yenye uozo wa kijamii kama vile ndoa, mapenzi, dini, utamaduni na falsafa kuhusu maisha. Tumeonyesha narnna maudhui ya uozo kijamii yalivyojengwa kifani na mafunzo waliyotoa watunzi. Sura ya tatu imejadili uchambuzi wa mashairi yenye maudhui ya uozo wa kisiasa. Tumeonyesha jinsi maudhui haya ya watunzi hawa yalivyosababisha uteuzi maalum wa lugha katika kuyaibusha. Sura ya nne imejihusisha na uchambuzi wa mashairi yenye maudhui ya uozo wa kiuchumi. Katika sehemu hii, tumeonyesha jinsi mtindo maalum wa mwandishi unavyosadia kuibusha ujumbe wake na mafunzo wanayotoa waandishi kurekebisha hali ya uozo. Sura ya tano ni hitimisho. Sura hii ni muhtasari wa matokeo ya utafiti wetu ambamo licha ya kueleza ugunduzi wa uchambuzi wetu tumetoa kauli yetu juu ya umuhimu wa utafiti wetu na maeneo ambayo yanastahili kufanyiwa utafiti zaidi hapo baadaye.en_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/14205
dc.language.isootheren_US
dc.titleUchunguzi wa uozo katlka mashairi ya Khatib na King'eien_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Uchunguzi wa uozo katlka mashairi ya Khatib na King'ei.pdf
Size:
53.12 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full text thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: