Uchunguzi wa uozo katlka mashairi ya Khatib na King'ei
Loading...
Date
2015-12
Authors
Barasa, Ayub O.
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia uozo katika mashairi ya Khatib na King'ei kwa kuongozwa
na nadharia ya kimtindo na maadili. Nadharia hizi zilifaa utafiti huu ikizingatiwa
kwamba maudhui ya mtunzi na mtindo anaoutumia katika kutoa ujumbe wake ni
vipengele vinavyotegemeana. Mtunzi hutunga kutokana na tajriba aliyopata katika
mazingira yake na lugha ndiyo aitumiayo kueleza mambo mbalimbali ya jamii yake kwa
njia ya kubuni.
Tasnifu hii ina sura tano. Sura ya kwanza imetupa mwelekeo wa utafiti, malengo ya
utafiti na sababu za kuchagua mada. Hali kadhalika sura hii imeshughulikia misingi ya
nadharia, upeo na mipaka na yaliyoandikwa kuhusu mada. Mwisho ni mbinu za utafiti na
uchanganuzi wa data.
Sura ya pili imejadili mashairi yenye uozo wa kijamii kama vile ndoa, mapenzi, dini,
utamaduni na falsafa kuhusu maisha. Tumeonyesha narnna maudhui ya uozo kijamii
yalivyojengwa kifani na mafunzo waliyotoa watunzi.
Sura ya tatu imejadili uchambuzi wa mashairi yenye maudhui ya uozo wa kisiasa.
Tumeonyesha jinsi maudhui haya ya watunzi hawa yalivyosababisha uteuzi maalum wa
lugha katika kuyaibusha.
Sura ya nne imejihusisha na uchambuzi wa mashairi yenye maudhui ya uozo wa
kiuchumi. Katika sehemu hii, tumeonyesha jinsi mtindo maalum wa mwandishi
unavyosadia kuibusha ujumbe wake na mafunzo wanayotoa waandishi kurekebisha hali
ya uozo.
Sura ya tano ni hitimisho. Sura hii ni muhtasari wa matokeo ya utafiti wetu ambamo licha
ya kueleza ugunduzi wa uchambuzi wetu tumetoa kauli yetu juu ya umuhimu wa utafiti
wetu na maeneo ambayo yanastahili kufanyiwa utafiti zaidi hapo baadaye.
Description
Department of Kiswahili and African Languages, 111p. Dec.2015, The PL 8704 .U3B3