Fonolojia ya utohozi wa manenomkopo ya Ekegusii kutoka Kiswahili

dc.contributor.advisorThuo, A.D.M.
dc.contributor.advisorAbdul, Farida
dc.contributor.authorMogaka, Roda
dc.date.accessioned2011-11-08T13:17:31Z
dc.date.available2011-11-08T13:17:31Z
dc.date.issued2011-11-08
dc.descriptionThe PL 8224.M6en_US
dc.description.abstractUfafiti huu umechanganua taratibu za utohozi wa manenomkopo ya Ekegusii kutoka Kiswahili kwa madhumuni ya kubainisha kanuni zinazohusika. Uchanganuzi umeongozwa na mtazamo wa Fonolojia Tenganishi ambao ni mojawapo ya mtaazamo ya Fonolojia Zalishi. Kulingana na mtazamo huu, fonolojia ni mfumo sauti wenye rusu nne: rusu msingi, rusu fonimu, rusu silabi na rusu toni. Data msingi ya utafiti ilikusanywa kupitia mbinu ya uchunguzi wa kushiriki na kusikiliza ambapo mazungumzo ya nyanja mbalimbali yalisikilizwa. Katika uwasilishi, maelezo yameambatana na michoro sahili, michoro matawi na majedwali. Utafiti huu una sura nne. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti ambao umeshughulikia swala la utafiti, malengo ya utafiti, tahadhania, upeo na mipaka, misingi ya nadharia na mbinu za utafiti. Katika sura ya pili vigezo vya fonolojia ya Ekegusii ambavyo ni fonimu za vokah na konsonanti, silabi na sifa arudhi zimebainishwa. Sura ya tatu imemulika taratibu za utohozi wa fonimu, silabi na sifa arudhi. Hatimaye sura ya nne imeangazia matokeo ya utafiti na mapendekezo. Matokeo ya utafiti yanaonyesha utohozi wa manenomkopo huongozwa na kudhibitiwa na kanuni na sheria za fonolojia ya Ekegusii. Hatimaye uchunguzi umetoa mapendekezo ya tafiti zaidi katika fonolojia ya Ekegusii. Utafiti huu una nafasi ya kuchangia uwanja wa isimu za lugha za Kiafrika kwa jumla tukizingatia kwamba utohozi unaweza kutumika katika kulinganisha mifano ya fonolojia. Pamoja na hayo data na matokeo ya uchanguzi yanaweza kuwasaidia wasomi wa isimu za lugha za Kiafrika.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/1614
dc.language.isoenen_US
dc.subjectGusii language--Foreign elements..Gusii language--Foreign words and phrases//Swahili language--Kenya //Bantu languagesen_US
dc.titleFonolojia ya utohozi wa manenomkopo ya Ekegusii kutoka Kiswahilien_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Fonolojia ya utohozi wa manenomkopo ya Ekegusii....pdf
Size:
59.73 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full text Thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
2.68 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: