Fonolojia ya utohozi wa manenomkopo ya Ekegusii kutoka Kiswahili

Loading...
Thumbnail Image
Date
2011-11-08
Authors
Mogaka, Roda
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Ufafiti huu umechanganua taratibu za utohozi wa manenomkopo ya Ekegusii kutoka Kiswahili kwa madhumuni ya kubainisha kanuni zinazohusika. Uchanganuzi umeongozwa na mtazamo wa Fonolojia Tenganishi ambao ni mojawapo ya mtaazamo ya Fonolojia Zalishi. Kulingana na mtazamo huu, fonolojia ni mfumo sauti wenye rusu nne: rusu msingi, rusu fonimu, rusu silabi na rusu toni. Data msingi ya utafiti ilikusanywa kupitia mbinu ya uchunguzi wa kushiriki na kusikiliza ambapo mazungumzo ya nyanja mbalimbali yalisikilizwa. Katika uwasilishi, maelezo yameambatana na michoro sahili, michoro matawi na majedwali. Utafiti huu una sura nne. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti ambao umeshughulikia swala la utafiti, malengo ya utafiti, tahadhania, upeo na mipaka, misingi ya nadharia na mbinu za utafiti. Katika sura ya pili vigezo vya fonolojia ya Ekegusii ambavyo ni fonimu za vokah na konsonanti, silabi na sifa arudhi zimebainishwa. Sura ya tatu imemulika taratibu za utohozi wa fonimu, silabi na sifa arudhi. Hatimaye sura ya nne imeangazia matokeo ya utafiti na mapendekezo. Matokeo ya utafiti yanaonyesha utohozi wa manenomkopo huongozwa na kudhibitiwa na kanuni na sheria za fonolojia ya Ekegusii. Hatimaye uchunguzi umetoa mapendekezo ya tafiti zaidi katika fonolojia ya Ekegusii. Utafiti huu una nafasi ya kuchangia uwanja wa isimu za lugha za Kiafrika kwa jumla tukizingatia kwamba utohozi unaweza kutumika katika kulinganisha mifano ya fonolojia. Pamoja na hayo data na matokeo ya uchanguzi yanaweza kuwasaidia wasomi wa isimu za lugha za Kiafrika.
Description
The PL 8224.M6
Keywords
Gusii language--Foreign elements..Gusii language--Foreign words and phrases//Swahili language--Kenya //Bantu languages
Citation