Athari ya duksi katlka ufunzaji na ujifunzaji wa kiswahili: mtazamo wa uchanganuzi linganishi tasnifu

dc.contributor.advisorKing'ei, Kitula
dc.contributor.advisorOsore, Miriam
dc.contributor.authorWenyaa, Nasaba Salome
dc.date.accessioned2016-01-27T05:46:55Z
dc.date.available2016-01-27T05:46:55Z
dc.date.issued2007
dc.descriptionIliyotolewa kwa madhumuni ya kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili katlka chuo kikuu cha Kenyatta, 2007en_US
dc.description.abstractKazi hii imekusudia kuchanganua athari ya elimu ya Duksi katika ufunzaji na ujifunzaji wa sarufi ya lugha ya Kiswahili kwa mujibu wa mtazamo wa nadharia ya Uchanganuzi Linganishi. Vipengele vya kisarufi yaani abjadi, maendelezo, msamiati, mtindo wa kuandika, mpangilio wa maneno katika sentensi ndivyo vilivyochunguzwa katika utafiti huu. Sampuli mseto ndiyo iliyochaguliwa na kuhusishwa. Watafiti walioshirikishwa walitoka katika wilaya ya Garissa, mjini pamoja na viunga vyake. Tajriba, imani, elimu, mielekeo na maoni ya wanajamii wa viwango mbalimbali yalizingatiwa. Kazi hii pia ilizingatia mbinu za kufunzia Kiswahili madhumuni yakiwa ni kuboresha na kuimarisha ufunzaji na ujifunzaji wa lugha hii katika mkabala wa mazingira ambapo lugha ya Kiarabu inazingatiwa. Yaani hutumiwa kwa kuendeshea shughuli za kidini. Kutokana na utafiti huu ilibainika kuwa elimu ya Duksi ina athari chanya na hasi. 'Mbinu za kufunzia zimedhihirisha njia tofauti tofauti zinazoweza kusaidia kuinua kiwango cha kufunza lugha. Papo hapo kutokana na ukinzano kati ya vipengele vya kisarufi vya (Kiarabu na Kiswahili), imetambulikana kuwa wanafunzi hupata shida zinazohusiana na abjadi, maendelezo, hijai, msamiati na maana ya sentensi. Utafiti huu umependekeza kuwa bado Kuna haja ya kuendeleza elimu jumuifu. ambapo mbinu changamano zinaweza kutumika. Hii ni kwa sababu mafunzo hayo yote ya kidini na ya kimagharibi yana manufaa kwa maisha ya wanafunzi wakiwa shuleni na hata baada ya masomo shuleni.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/14084
dc.language.isoenen_US
dc.titleAthari ya duksi katlka ufunzaji na ujifunzaji wa kiswahili: mtazamo wa uchanganuzi linganishi tasnifuen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Athari ya duksi katlka ufunzaji na ujifunzaji wa kiswahili mtazamo wa uchanganuzi linganishi.pdf
Size:
67.49 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Thesis Full text
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: