Maudhui ya Ukungwi katika Nyimbo Teule za Taarab

Loading...
Thumbnail Image
Date
2025-07
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
East African Journal of Swahili Studies
Abstract
Nyimbo za taarab zimetafitiwa na wataalam mbalimbali kwa mitazamo tofautitofauti. Kutokana na uchunguzi wa kina wa mtafiti, inabainika kuwa tafiti za awali kuhusu nyimbo za taarab, zimeegemezwa kwenye uchunguzi wa mafumbo katika taarab, masuala ya itikadi, nafasi ya mwanamke katika nyimbo za taarab usimulizi pamoja na uchanganuzi wa taswira katika nyimbo za taarab. Swala la jumbe za nyimbo za taarab kufungamana na mambo ya kijamii yakiwemo utamaduni limetajwa tu kijuujuu katika tafiti zao. Kutokana na upeku zi wa kina wa mtafiti, hakuna utafiti ambao umefanywa kuhusu dhima ya kungwi inavyotekelezwa na baadhi ya nyimbo za taarab. Utafiti huu ulihusu ubainishaji wa maudhui ya ukungwi katika nyimbo teule za taarab. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Simiotik i. Nadharia hii iliasisiwa na Ferdinand Dessaussure (1983) na Charles Pierce (1998) na inahusu uhusiano uliopo kati ya kitaja na kitajwa na matumizi ya ishara, picha na msimbo. Nguzo hii ilisaidia katika kufafanua mbinu za uwasilishaji wa ujumbe katika n yimbo teule za taarab. Data ya kimsingi iliyoichanganuliwa ilikuwa ya maktabani ambapo mtafiti alipakua nyimbo teule kutoka kwenye mtandao wa You Tube na kuzichanganua kwa kina. Matokeo yalionyesha kuwa kungwi ana jukumu la kuwafundisha wanawari kuhusu mas uala ya unyumba yakiwemo usafi wa mwili na nyumba, namna ya kumhudumia mume, namna ya kusema na marafiki na jamaa za mume, matumizi ya vifaa vya kiasili kama vile mbuzi, kinu, mchi ufagio miongoni mwa mengine. Aidha, maudhui haya ya ukungwi yanafundishwa n a waimbaji wa nyimbo teule za taarab
Description
Article
Keywords
Citation
Wendo, F. H. & Titus, K.(2025). Maudhui ya Ukungwi katika Nyimbo Teule za Taarab.East African Journal of Swahili Studies, 8(2), 119-132. https://doi.org/10.37284/jammk.8.2.3347