Kuchunguza ufundishaji wa kusoma kwa sauti katika madarasa ya kwanza, pili na katika shule za msingi

dc.contributor.authorOkoba, Beatrice Wambui
dc.date.accessioned2011-11-14T09:54:24Z
dc.date.available2011-11-14T09:54:24Z
dc.date.issued2011-11-14
dc.descriptionThe PL 8702 .O39K8en_US
dc.description.abstractUtafiti huu umeshughulikia kuchunguza ufundishaji wa kusoma kwa sauti katika madarasa ya chini katika shule za msingi. Utafiti huu ulilenga kuonyesha mbinu na nyenzo zilizotumiwa katika kutekeleza ufunzaji wa kusoma kwa sauti. Aidha, vitabu na tathmini zilichunguzwa na kuonyesha mchango wake katika kuimarisha usomaji. Kadhalika, matatizo yaliyowakabili watoto katika usomaji yaliangaziwa na ufaafu wa mikakati iliyotumiwa na walimu. Utafiti ulinuia kuonyesha matatizo katika stadi ya kusoma na kuchunguza mikakati iliyotumiwa na walimu kukabiliana na changamoto hizi. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Krashen pamoja na Modeli Husishi. Nadharia ya Krashen inaeleza uzingativu wa taratibu mbalimbali ili kufanikisha ujifunzaji kusoma L2. Nayo, modeli Husishi inasisitiza umuhimu wa kukuza ujuzi wa kupambanua sauti na ufahamu wa maana ya sauti hizo kwa pamoja. Ili kufanikisha malengo ya utafiti, walimu walijaza hojaji na uchunguzi wa darasani ulifanywa ili kuchunguza utekelezaji wa funzo la. kusoma kwa sauti. Walimu waliteuliwa kutoka shule sita za umma katika tarafa ya Gatanga, wilaya ya Thika. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha kuwa watoto walikosa msingi mzuri katika stadi hii. Watoto wengi waliendelea na madarasa ya juu kabla ya kuimarika katika vipengele vya kimsingi katika stadi ya kusoma kwa jumla. Imedhihirika kuwa walimu katika madarasa haya wanahitaji kuhamasishwa zaidi kuhusu hatua za kusoma zinavyofanyika. Hii ni kwa sababu baadhi ya walimu walikosa ubunifu katika utekelezaji wa shughuli za darasani katika stadi ya kusoma kwa sauti.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/1636
dc.language.isoenen_US
dc.subjectSwahili language -- Study and teaching -- Kenya//Reading(Primary) -- Research -- Study and teaching -- Kenya//Oral readingen_US
dc.titleKuchunguza ufundishaji wa kusoma kwa sauti katika madarasa ya kwanza, pili na katika shule za msingien_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Kuchunguza ufundishaji wa kusoma kwa sauti katika madarasa ya kwanza, pili na tatu katika.....pdf
Size:
73.65 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Thesis full text
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
2.68 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: