Kuchunguza ufundishaji wa kusoma kwa sauti katika madarasa ya kwanza, pili na katika shule za msingi
Loading...
Date
2011-11-14
Authors
Okoba, Beatrice Wambui
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia kuchunguza ufundishaji wa kusoma kwa sauti katika madarasa ya chini katika shule za msingi. Utafiti huu ulilenga kuonyesha mbinu na nyenzo zilizotumiwa katika kutekeleza ufunzaji wa kusoma kwa sauti. Aidha, vitabu na tathmini zilichunguzwa na kuonyesha mchango wake katika kuimarisha usomaji. Kadhalika, matatizo yaliyowakabili watoto katika usomaji yaliangaziwa na ufaafu wa mikakati iliyotumiwa na walimu. Utafiti ulinuia kuonyesha matatizo katika stadi ya kusoma na kuchunguza mikakati iliyotumiwa na walimu kukabiliana na changamoto hizi. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Krashen pamoja na Modeli Husishi. Nadharia ya Krashen inaeleza uzingativu wa taratibu mbalimbali ili kufanikisha ujifunzaji kusoma L2. Nayo, modeli Husishi inasisitiza umuhimu wa kukuza ujuzi wa kupambanua sauti na ufahamu wa maana ya sauti hizo kwa pamoja. Ili kufanikisha malengo ya utafiti, walimu walijaza hojaji na uchunguzi wa darasani ulifanywa ili kuchunguza utekelezaji wa funzo la. kusoma kwa sauti. Walimu waliteuliwa kutoka shule sita za umma katika tarafa ya Gatanga, wilaya ya Thika. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha kuwa watoto walikosa msingi mzuri katika stadi hii. Watoto wengi waliendelea na madarasa ya juu kabla ya kuimarika katika vipengele vya kimsingi katika stadi ya kusoma kwa jumla. Imedhihirika kuwa walimu katika madarasa haya wanahitaji kuhamasishwa zaidi kuhusu hatua za kusoma zinavyofanyika. Hii ni kwa sababu baadhi ya walimu walikosa ubunifu katika utekelezaji wa shughuli za darasani katika stadi ya kusoma kwa sauti.
Description
The PL 8702 .O39K8
Keywords
Swahili language -- Study and teaching -- Kenya//Reading(Primary) -- Research -- Study and teaching -- Kenya//Oral reading