Lugha ya wanawake wakikuyu inavyoimarishwa ubabedume katika maongezi ya kawaida

dc.contributor.advisorAlice Nyambura Mwihaki
dc.contributor.advisorMiriam Kenyani Osore
dc.contributor.authorMuchiri, Patrick Maina
dc.date.accessioned2012-03-29T06:26:37Z
dc.date.available2012-03-29T06:26:37Z
dc.date.issued2012-03-29
dc.descriptionDepartment of Kiswahili and African Languages,151p.The PL 8379 .M8 2011
dc.description.abstractUtafiti huu ulilenga kubainishajinsi wanawake Wakikuyu wanavyouimarisha ubabedume kupitia maongezi yao ya kawaida. Nadharia ya Tahakiki Usemi imekuwa nanga ya uchanganuzi wa matumizi ya lugha kutokana na msisitizo wake wa muktadha katika kueleweka kwa matamshi. Sarufi Amilishi Mfumo imejaliza uchanganuzi kupitia msisitizo wake wa mfumo wa maana za matamshi. Utafiti ulifanywa maktabani na pia nyanjani. Maktabani, data ya upili ilitumiwa ili kufanikisha utafiti wa nyanjani. Nyanjani, maongezi halisi ya wanawake kuhusu wanaume yalizingatiwa hasa sokoni, na kwenye vikundi vya wanawake. Uwasilishaji wa data utakuwa wa kimaelezo kupitia sura tano. Sura ya kwanza imejenga utangulizi ikihusisha vipengele vya kimsingi vya utafiti. Utamadunijamii wa Wakikuyu umeshughulikiwa katika sura ya pili pamoja na vipengele vyake vinavyokuza ubabedume. Taswira ya mwanamume na taswira ya mwanamke zimefafanuliwa na mifano halisi ya kimaongezi kutolewa katika sura ya tatu na ya nne mtawalia. Ufafanuzi wa maana za taswira hizi ulikitwa katika miktadha ya matumizi ya lugha kama inavyoelekeza nadharia inayotumiwa katika utafiti huu. Sura ya tano imehitimisha utafiti kwa kutoa matokeo ya utafiti, mahitimisho ya utafiti pamoja na mapendekezo ya utafiti zaidi. Utafiti huu unatarajiwa kuwanufaisha wanaisimu, wasomi wa masuala ya kijinsia, na wanawake kwa jumla. Pia unatarajiwa kusaidia katika uzinduzi wa jamii kuhusu matumizi ya lugha na athari zake kimawasiliano.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/3584
dc.language.isoenen_US
dc.subjectKikuyu(African Language)
dc.titleLugha ya wanawake wakikuyu inavyoimarishwa ubabedume katika maongezi ya kawaidaen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Muchiri, Patrick Maina.pdf
Size:
45.65 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Abstract
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
2.68 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: