Lugha ya wanawake wakikuyu inavyoimarishwa ubabedume katika maongezi ya kawaida

Loading...
Thumbnail Image
Date
2012-03-29
Authors
Muchiri, Patrick Maina
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu ulilenga kubainishajinsi wanawake Wakikuyu wanavyouimarisha ubabedume kupitia maongezi yao ya kawaida. Nadharia ya Tahakiki Usemi imekuwa nanga ya uchanganuzi wa matumizi ya lugha kutokana na msisitizo wake wa muktadha katika kueleweka kwa matamshi. Sarufi Amilishi Mfumo imejaliza uchanganuzi kupitia msisitizo wake wa mfumo wa maana za matamshi. Utafiti ulifanywa maktabani na pia nyanjani. Maktabani, data ya upili ilitumiwa ili kufanikisha utafiti wa nyanjani. Nyanjani, maongezi halisi ya wanawake kuhusu wanaume yalizingatiwa hasa sokoni, na kwenye vikundi vya wanawake. Uwasilishaji wa data utakuwa wa kimaelezo kupitia sura tano. Sura ya kwanza imejenga utangulizi ikihusisha vipengele vya kimsingi vya utafiti. Utamadunijamii wa Wakikuyu umeshughulikiwa katika sura ya pili pamoja na vipengele vyake vinavyokuza ubabedume. Taswira ya mwanamume na taswira ya mwanamke zimefafanuliwa na mifano halisi ya kimaongezi kutolewa katika sura ya tatu na ya nne mtawalia. Ufafanuzi wa maana za taswira hizi ulikitwa katika miktadha ya matumizi ya lugha kama inavyoelekeza nadharia inayotumiwa katika utafiti huu. Sura ya tano imehitimisha utafiti kwa kutoa matokeo ya utafiti, mahitimisho ya utafiti pamoja na mapendekezo ya utafiti zaidi. Utafiti huu unatarajiwa kuwanufaisha wanaisimu, wasomi wa masuala ya kijinsia, na wanawake kwa jumla. Pia unatarajiwa kusaidia katika uzinduzi wa jamii kuhusu matumizi ya lugha na athari zake kimawasiliano.
Description
Department of Kiswahili and African Languages,151p.The PL 8379 .M8 2011
Keywords
Kikuyu(African Language)
Citation