Wakaa katika Hotuba Teule za Wanasiasa wa Kenya

dc.contributor.authorMukonambi, Kekonen Stanley
dc.contributor.authorKaui,Titus
dc.date.accessioned2025-10-06T11:37:54Z
dc.date.available2025-10-06T11:37:54Z
dc.date.issued2025-08
dc.descriptionArticle
dc.description.abstractMakala hii inachunguza ubainishaji wa wakaa katika hotuba teule za wanasiasa wa Kenya. Baadhi ya wanasiasa hutoa hotuba zinazovuta makini ya wasikilizaji na wafuasi wao kwa mitindo tofauti. Mojawapo wa mbinu hii ya kimtindo ni usimulizi. Wakaa ni mojawapo wa kipengele cha kimtindo katika usimulizi. Tafiti kadha zimefanywa kubainisha wakaa na matumizi yake katika tanzu za fasihi andishi na fasihi simulizi (taz. Kwaka; 2015; Khamis; 2015; Muiya; 2018; Kinga; 2020; Asige, 2021). Licha ya hayo, tafiti hizi za awali hazikushughulikia wakaa kwa kuhusisha moja kwa moja si hotuba tu bali hotuba za kisiasa. Ni katika msingi huu ndipo makala hii imechunguza jinsi wakaa inavyojitokeza katika hotuba teule za wanasiasa wa Kenya. Makala hii imeelekezwa na nadharia ya Naratolojia iliyoasisiwa na mwanafalsafa Plato katika chapisho lake The Republic na baadaye ikaendelezwa na mwanafunzi wake Aristotle (1920) aliyewasilisha mawazo yake katika chapisho la The Poetics na wananaratolojia wa hivi majuzi Gennette (1980), Prince (1982) na Rimmon-Kenan (2002). Uchunguzi huu ulizingatia mawazo yake Rimmon-Kenan. Naratolojia ni stadi ya aina ya utendaji kazi wa usimulizi. Huangalia undani wa vifaa vinavyoongoza maelezo ya simulizi na ufahamu wa utendaji kazi wake. Data iliyotumika katika makala hii imetokana na kusoma machapisho maktabani kama vile tasnifu, majarida na vitabu. Halikadhalika, utazamaji, usikilizaji na uchambuzi wa hotuba teule za wanasiasa Mhes. Kenyatta, Odinga na Ruto katika mtandao wa YouTube ulihusishwa. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha kuwepo kwa vipengele vya wakaa vya mpangilio, muda na idadi au umara katika hotuba za wanasiasa. Isitoshe, imebainika kuwa kipengele hiki cha usimulizi kimetumiwa kuendeleza maudhui, fani za lugha na kuchimuza wahusika.
dc.identifier.citationStanley, M. K. & Kaui, T. (2025). Wakaa katika Hotuba Teule za Wanasiasa wa Kenya. East African Journal of Swahili Studies, 8(2), 173-187. https://doi.org/10.37284/jammk.8.2.3485
dc.identifier.urihttps://doi.org/10.37284/jammk.8.2.3485
dc.identifier.urihttps://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/31570
dc.language.isoen
dc.publisherEast African Journal of Swahili Studies
dc.titleWakaa katika Hotuba Teule za Wanasiasa wa Kenya
dc.typeArticle
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Full-text Journal Article.pdf
Size:
431.54 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
2.66 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: