Uamilifu wa Tonisho Katika Sentensi za Kikamba

dc.contributor.advisorKing'ei, Kitula Osore, Miriam
dc.contributor.authorMuinde, Sarah Nthenya
dc.date.accessioned2016-04-21T09:25:30Z
dc.date.available2016-04-21T09:25:30Z
dc.date.issued2009
dc.descriptionDepartment of Kiswahili and African Languages, 143p. 2009en_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulitekelezwa kwa madhumuni ya kuchambua na kujadili ruwaza za tonisho katika sentensi za Kikamba, ili kubainisha muundo na uamilifu katika nyanja za sintaksia na pragmatiki. Uchanganuzi ulitegemea mihimili ya Sarufi Amilifu Mfumo, hasa amali za lugha, tanzu za kisarufi na mitazamo ya kishazi. Nadharia ya Sarufi Amilifu Mfumo ilishirikisha misingi ya kimuundo ya Sarufi Zalishi. Swala la utafiti lilikuwa kudhihirisha uamilifu wa tonisho katika sentensi za Kikamba kupitia dhima za kisintaksia na kipragmatiki. Mbinu za utafiti zilijumuisha nyanjani na maktabani. Matokeo ya utafiti yaliwakilishwa kwa njia ya maelezo katika sura nne. Sura ya kwanza ilichambua usuli wa mada na kubainisha suala la utafiti, malengo na tahakiki za utafiti, misingi ya kuchagua mada, tahakiki ya maandishi, misingi ya kinadharia na mbinu za utafiti. Sura ya pili ilifafanua muundo wa sentensi za Kikamba. Dhima kuu ya sura hii ilikuwa kutambulisha maneno na kuchanganua miundo virai vyake, kwa madhumuni ya kuwakilisha sentensi za Kikamba. Uchanganuzi wa kishazi ulifanywa kupitia mitazamo mitatu ya kishazi. Ruwaza za tonisho katika hivi vishazi zilibainishwa kwa mujibu wa maana na uamilifu wake katika sura ya tatu. Tonisho ni kigezo muhimu katika sarufi ya Kikamba na ina mchango katika uwanja wa sintaksia kwa jumla pamoja na utumikizi katika ufundishaji wa lugha.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/14619
dc.language.isoenen_US
dc.publisherKenyatta Universityen_US
dc.titleUamilifu wa Tonisho Katika Sentensi za Kikambaen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Uamilifu wa tonisho katika sentensi za kikamba.....pdf
Size:
55.61 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full Text Thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: