Uhalisiajabu katika riwaya ya babu alipofufuka (2001) ya S.A mohamed na bina-adamu! (2002) yA K.W Wamitila

dc.contributor.advisorKing'ei, Kitula Osore, Miriam
dc.contributor.authorMagaju, Jacinta Kagendo
dc.date.accessioned2017-12-01T13:18:45Z
dc.date.available2017-12-01T13:18:45Z
dc.date.issued2004-08
dc.descriptionTasnifu hii imetolewa iIi kutosheleza baadhi ya mahitaji ya Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta. Agosti 2004en_US
dc.description.abstractUtafiti huu umeshughulikia swala la uhalisiajabu katika riwaya teule za fasihi ya Kiswahili. Riwaya zilizohakikiwa ni Babu Alipofufuka (2001) ya S.A. Mohamed na Bina-Adamu! (2002) ya K.W. Wamitila. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni kitengo kimoja cha mwelekeo wa usasaleo. Hii ni nadharia ya uhalisiajabu. Katika nadharia ya uhalisiajabu, matukio yanasawiriwa kiajabuajabu, ni ya kuogofya na kutisha. Matukio haya huashiria hali halisi ya maisha katika jamii. Uhalisiajabu ni mtindo wa riwaya wa hivi majuzi unaopiku njia za kimapokeo za uandishi wa fasihi ya Kiswahili na usawiri wa jamii. Kimapokeo, riwaya inapaswakujengeka katika misingi ya uhalisia. Tasnifu hii ina jumla ya sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti. Hapa ndipo tumeshughulikia mada ya utafiti, malengo ya utafiti, sababu za kuchagua mada na yaliyoandikwa kuhusu hii mada. Aidha, tumejadili upeo wa utafiti huu na misingi ya nadharia iliyouongoza. Mwisho, mbinu za utafiti zimeelezwa. Sura ya pili imejadili maisha ya waandishi S.A. Mohamed na K.W. Wamitila. Tumeonyesha vipindi mbalimbali vya uandishi wao. Uchunguzi huu umedhamiria kuonyesha mitindo waliyoitumia tangu waanze kuandika na pia kuonyesha ni kwenye kipindi gani cha uandishi waliingilia uandishi wa kihalisiajabu na kwa nini walifanya hivyo. Sura ya tatu na nne zinachunguza jinsi riwaya za Babu Alipofufuka na Bina-Adamu! zimetumia uhalisiajabu katika kuwasilisha ujumbe. Tumeonyesha mihimili ya nadharia ya uhalisiajabu waliyoitumia. Mihimili hii ni pamoja na matukio ya kiajabuajabu, ndoto na uhalisia, uduara wa wakati, visaasili, uvunjwaji wa mipaka ya mahali na upekee wa mtindo wa riwaya ya kihalisiajabu. ,;~ Sura ya tano imehusika na kulinganisha na kulinganua riwaya zote mbili kwa mujibu wa mada husika. Aidha, matokeo ya utafiti, matatizo yaliyokabiliwa katika utafiti na mapendekezo yametolewa katika sura hii. Kutokana na utafiti huu, imebainika wazi kwamba Mohamed na Wamitila wanatumia uhalisiajabukimakusudi. Mihimili mikuu ya uhalisiajabu imo katika kazi zao. La maana zaidi ni kwamba wanatumia uhalisiajabu kama mkakati unaowawezesha kujadili maswala yanayousibu ujirani wetu. S.A. Mohamed anatumia mkakati huu kumulika rnatatizo ya kiuchumi na ya kijamii yanayowakabili Waafrika kutokana na utawala finyu wa viongozi wao. K.W. Wamitila anatumia mtindo huo huo kuupiga vita utandaradhi na ubepari wa kimataifa. Pamoja na kuonyesha matatizo yanayoyakabiliwa na Waafrika, Mohamed na Wamitila wana imani kwamba matatizo ya Waafrika yanaweza kutatuliwa si kwa kutafuta tiba huko nje katika mataifa ya Kimagharibi, bali kwa kuyatafuta humuhumu barani Afrika kihalisiajabu.en_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/17893
dc.language.isootheren_US
dc.publisherKenyatta Universityen_US
dc.subjectMohamed, S.A., Babu alipofufukaen_US
dc.subjectWamitila, K.W., Bina-adamuen_US
dc.subjectHistory and criticismen_US
dc.titleUhalisiajabu katika riwaya ya babu alipofufuka (2001) ya S.A mohamed na bina-adamu! (2002) yA K.W Wamitilaen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Uhalisiajabu katika riwaya.pdf
Size:
76.63 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full text thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: