• English
    • français
  • English 
    • English
    • français
  • Login
View Item 
  •   Repository Home
  • Master Theses and Dissertations(MST)
  • MST-School of Humanities and Social Sciences
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • View Item
  •   Repository Home
  • Master Theses and Dissertations(MST)
  • MST-School of Humanities and Social Sciences
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • View Item
JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

Ufundi katika riwaya za Mohammed Said Abdulla

Thumbnail
View/Open
Full text thesis (56.32Mb)
Date
2012-05-09
Author
Kamau, Margaret
Metadata
Show full item record
Abstract
Tasnifu hii imejadili ufundi katika riwaya za Mohammed Said Abdulla. Kazi hii inajaribu kuonyesha ufundi alioutumia mwandishi katika kuwasilisha ujumbe wake. Sura ya kwanza ni utangulizi was utafiti wetu. Hapa tumejadili somo la utafiti, madhumuni ya utafiti, upeo na pia sababu za kulichagua somo hili. Hali kadhalika tumegusia yale yaliyoandikwa na wengine kuhusu somo hili pamoja na machache kuhusu nadharia inayotuongoza katika uchunguzi wetu. Mwisho tumejadili njia za utafiti ambazo tumetumia kufanikisha utafiti wetu. Sura ya pili inaangalia maisha ya mwandishi ili kuona ni mambo yapi yalimwathiri katika utunzi wake. Sura hii pia yaangalia sifa za fasihi ya upelezi ili kusaidia msomaji kuelewa mkondo wa riwaya za mwandishi. Muhtasari wa vita alivyoandika mwandishi pia umetolewa katika sura hii. Sura ya tatu inajadili mbinu za unahishaji wa maana zilizotumiwa na mwandishi Abdulla. Tamathali zilizojadiliwa ni methali, misemo tashhisi na stiari. Tumebaini jinsi tamathali hizi zilivyotumiwa na mwandishi katika kuwasilisha ujumbe wake. Sura ya nne imejadili ubunifu katika kazi za mwandishi Abdulla. Tamathali tulizojadili ni takriri, mazungumzo, tabaini, lafidhi, maelezo, tashbihi na tanakali. Tmebaini jinsi tamathali hizi zilivyotumia kwa njia ya ubunifu kuleta ufasaha wa kazi ya sanaa na kufanya usomaji uwe na kuvutia. Sura ya tano ni hitimisho ya uchunguzi wetu. Katika sura hii tumetoa muhtasati wa kazi yetu kwa jumla na kuonyesha kwamba hata ingawa mwandishi hana maudhui mazito ametumia lugha kwa ufundi wa hali ya juu kisanaa. Zaidi ya hayo, tumejadili matatizo yaliyotukumba na kutoa mapendekezo ya maeneo yanayostahili kufanyiwa utafiti zaidi hapo baadaye.
URI
http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/4521
Collections
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages [234]

Designed by Library ICT Team copyright © 2017 
Contact Us | Send Feedback

 

 

Browse

All of RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

My Account

LoginRegister

Designed by Library ICT Team copyright © 2017 
Contact Us | Send Feedback