Ufundi katika riwaya za Mohammed Said Abdulla

dc.contributor.authorKamau, Margaret
dc.date.accessioned2012-05-09T08:30:01Z
dc.date.available2012-05-09T08:30:01Z
dc.date.issued2012-05-09
dc.descriptionThe PL 8704.U43 K3en_US
dc.description.abstractTasnifu hii imejadili ufundi katika riwaya za Mohammed Said Abdulla. Kazi hii inajaribu kuonyesha ufundi alioutumia mwandishi katika kuwasilisha ujumbe wake. Sura ya kwanza ni utangulizi was utafiti wetu. Hapa tumejadili somo la utafiti, madhumuni ya utafiti, upeo na pia sababu za kulichagua somo hili. Hali kadhalika tumegusia yale yaliyoandikwa na wengine kuhusu somo hili pamoja na machache kuhusu nadharia inayotuongoza katika uchunguzi wetu. Mwisho tumejadili njia za utafiti ambazo tumetumia kufanikisha utafiti wetu. Sura ya pili inaangalia maisha ya mwandishi ili kuona ni mambo yapi yalimwathiri katika utunzi wake. Sura hii pia yaangalia sifa za fasihi ya upelezi ili kusaidia msomaji kuelewa mkondo wa riwaya za mwandishi. Muhtasari wa vita alivyoandika mwandishi pia umetolewa katika sura hii. Sura ya tatu inajadili mbinu za unahishaji wa maana zilizotumiwa na mwandishi Abdulla. Tamathali zilizojadiliwa ni methali, misemo tashhisi na stiari. Tumebaini jinsi tamathali hizi zilivyotumiwa na mwandishi katika kuwasilisha ujumbe wake. Sura ya nne imejadili ubunifu katika kazi za mwandishi Abdulla. Tamathali tulizojadili ni takriri, mazungumzo, tabaini, lafidhi, maelezo, tashbihi na tanakali. Tmebaini jinsi tamathali hizi zilivyotumia kwa njia ya ubunifu kuleta ufasaha wa kazi ya sanaa na kufanya usomaji uwe na kuvutia. Sura ya tano ni hitimisho ya uchunguzi wetu. Katika sura hii tumetoa muhtasati wa kazi yetu kwa jumla na kuonyesha kwamba hata ingawa mwandishi hana maudhui mazito ametumia lugha kwa ufundi wa hali ya juu kisanaa. Zaidi ya hayo, tumejadili matatizo yaliyotukumba na kutoa mapendekezo ya maeneo yanayostahili kufanyiwa utafiti zaidi hapo baadaye.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/4521
dc.language.isoenen_US
dc.subjectSwahili literatureen_US
dc.titleUfundi katika riwaya za Mohammed Said Abdullaen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Ufundi katika riwaya za mohammed said abdulla.pdf
Size:
56.33 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full text thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
2.68 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: