Umatini katika vichekesho vya "Redykyulass"

Loading...
Thumbnail Image
Date
2012-04-03
Authors
Neyole, Nafula Eunice
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu unachanganua usemi katika maigizo ya Kiswahili ya kikundi kinachoitwa "Redykyulass". Lengo la uchanganuzi huu ni kubainisha ikiwa maigizo ya "Redykyulass" yanakubalika kama matini kwa mujibu wa nadharia ya umatini. Mtazamo wa Beaugrande na Dressler (1981) ndio unaotumiwa kutathmini umatini wa "Redykyulass". Vigezo vya: mshikamano, muwala, muktadha, kusudio, ukubalifu, ufahamishaji na mwingiliano wa matini vinatumiwa. Aidha, utafiti huu unanuia kubainisha namna vigezo hivi vinavyodhihirika katika matini. Sura ya kwanza ambayo ni utangulizi wa tasnifu inashungulikia swala la utafiti, sababu za kuchagua mada, madhumuni ya utafiti, upeo wa utafiti, yaliyoandikwa katika utafiti. Sura ya pili, tatu na nne zinachanganua data kwa kutumia vigezo vya umatini vilivyopendekezwa na Beaugrande na Dressler (1981). Sura ya tano ni muhtasari wa matokeo ya utafiti kwa ujumla. Mapendekezo ya utafiti mwingine unaoweza katika uwanja huu pia yameonyeshwa katika sura hii.
Description
Department of Kiswahili and African Languages, 158p. 2003
Keywords
Theater--public relations
Citation