Udhihirikaji wa Viambajengo Katizwa Katika Lugha ya Kiswahili
No Thumbnail Available
Date
2024
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Makala hii inachunguza udhihirikaji wa viambajengo katizwa katika Kiswahili. Viambajengo katizwa ni elementi za neno au kishazi ambazo hazipatikani katika usanjari mmoja kwa sababu elementi kutoka mofu au kirai kingine zimeingilia kati (Reinholtz, 1999). Hili hutokea wakati mofu kadhaa za kiambajengo kimoja zimetengwa au maneno kadhaa ya kirai kimoja yametengwa. Kwa mfano: “Rais alizungumza, bila shaka, juu ya siasa.” Katika sentensi hii, kitenzi na kielezi chake vilitengwa na taarifa nyingine. Nadharia ya Sarufi Miundo Virai Katizwa iliyozungumziwa na Harman (1963) iliongoza utafiti huu. Data ya makala hii ilikusanywa nyanjani ambapo wataalamu wa lugha ya Kiswahili walihojiwa kuhusu usahihi wa sentensi katizwa na hata kusaidia kuzalisha zingine. Mbinu ya usampulishaji wa kimaksudi ilitumika katika uteuzi wa sampuli. Data ya utafiti huu ilibaini aina mbili kuu za virai katizwa. Ilibainika kuwa viambajengo katizwa husababishwa na ukanushi wa baadhi ya vitenzi, ukanushi maradufu, njeo vishazi tegemezi na vishazi viongezi. Tafiti zingine zinaweza kufanywa kuhusu udhihirikaji wa viambajengo katizwa katika aina nyingine ya kirai kama vile kirai kihusishi au kirai kivumishi katika lugha ya Kiswahili au lugha nyingine
Description
Research Article
Keywords
Citation
Lucas, P., & Mwita, L. (2024). Udhihirikaji wa Viambajengo Katizwa Katika Lugha ya Kiswahili. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 514-524. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.2355