Urejeleano Katika Utunzi wa Kamusi za Kiswahili: Uchanganuzi Linganishi wa Kamusi Teule za Lugha Moja
Abstract
Utafiti huu ulichunguza jinsi kipengele cha urejeleano kilivyoshughulikiwa katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu Toleo la Tatu (2013), Kamusi Kuu ya Kiswahili (2015) na Kamusi Elezi ya Kiswahili (2016). Nadharia ya miundomedio (mediostructures) iliuelekeza utafiti huu, ambao ulilenga kubaini vipengele vya urejeleano katika kamusi teule, kulinganisha na kulinganua matumizi ya urejeleano katika kamusi hizo, kujadili athari ya urejeleano katika kamusi hizo na hatimaye kupendekeza, kutegemea matokeo ya utafiti, namna ya kuboresha urejeleano katika kamusi za Kiswahili za lugha moja. Asilimia kubwa ya utafiti ilifanywa maktabani kwa kunukuu vipengele vinavyofaa kuhusishwa kwa kurejelea kutoka katika kamusi teule, na nyanjani kupitia mahojiano. Wachapishaji na watumiaji wa kamusi walihojiwa na maoni yao kujumuishwa katika utafiti huu. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kuiegemeza kwenye mihimili ya nadharia ya miundomedio na matokeo kutolewa kwa njia ya maelezo. Utafiti huu utaleta mwanga mpya katika kukishughulikia kipengele cha urejeleano katika kamusi za Kiswahili za lugha moja.