Urejeleano Katika Utunzi wa Kamusi za Kiswahili: Uchanganuzi Linganishi wa Kamusi Teule za Lugha Moja

dc.contributor.advisorLeonard Chacha Mwitaen_US
dc.contributor.advisoriRERI Mbaabuen_US
dc.contributor.authorMaithulia, Mweteri Isaiah
dc.date.accessioned2021-10-29T10:39:36Z
dc.date.available2021-10-29T10:39:36Z
dc.date.issued2021
dc.descriptionTasnifu hii Imewasilishwa Kutosheleza baadhi ya mahitaji ya Shahada ya Uzamili katika Idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika, Shule ya Elimu,Chuo Kikuu cha Kenyatta, Mei 2021en_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulichunguza jinsi kipengele cha urejeleano kilivyoshughulikiwa katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu Toleo la Tatu (2013), Kamusi Kuu ya Kiswahili (2015) na Kamusi Elezi ya Kiswahili (2016). Nadharia ya miundomedio (mediostructures) iliuelekeza utafiti huu, ambao ulilenga kubaini vipengele vya urejeleano katika kamusi teule, kulinganisha na kulinganua matumizi ya urejeleano katika kamusi hizo, kujadili athari ya urejeleano katika kamusi hizo na hatimaye kupendekeza, kutegemea matokeo ya utafiti, namna ya kuboresha urejeleano katika kamusi za Kiswahili za lugha moja. Asilimia kubwa ya utafiti ilifanywa maktabani kwa kunukuu vipengele vinavyofaa kuhusishwa kwa kurejelea kutoka katika kamusi teule, na nyanjani kupitia mahojiano. Wachapishaji na watumiaji wa kamusi walihojiwa na maoni yao kujumuishwa katika utafiti huu. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kuiegemeza kwenye mihimili ya nadharia ya miundomedio na matokeo kutolewa kwa njia ya maelezo. Utafiti huu utaleta mwanga mpya katika kukishughulikia kipengele cha urejeleano katika kamusi za Kiswahili za lugha moja.en_US
dc.description.sponsorshipChuo Kikuu cha Kenyattaen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/22881
dc.language.isootheren_US
dc.publisherKenyatta Universityen_US
dc.subjectUrejeleanoen_US
dc.subjectUtunzien_US
dc.subjectKamusien_US
dc.subjectKiswahilien_US
dc.subjectUchanganuzi Linganishien_US
dc.subjectKamusi Teuleen_US
dc.subjectLugha Mojaen_US
dc.titleUrejeleano Katika Utunzi wa Kamusi za Kiswahili: Uchanganuzi Linganishi wa Kamusi Teule za Lugha Mojaen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Urejeleano Katika .....pdf
Size:
939.16 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full text thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: