Uchanganuzi wa Kimofosintaksia wa Viangami Katika Lugha ya Kiswahili
Loading...
Date
2021
Authors
Ndumba, Kimonye Naomi
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Lengo la utafiti huu ni kushughulikia uchanganuzi wa kimofosintaksia wa
viangami katika lugha ya Kiswahili. Utafiti huu ulilenga kuthihirisha kuwa kuna
aina tofauti za viangami katika lugha ya Kiswahili. Viangami ni mofimu
zinazojisimamia kisintaksia lakini kifonolojia ni tegemezi. Viangami hutegemea
neno kuu kifonolojia. Viangami huambishwa kwa neno kuu. Kiangami ni sehemu
ya neno kamili inayochukua nafasi ya kiambishi. Utafiti ulilenga kuchunguza
changamoto katika uainishaji wa maneno yenye viangami, tofauti zilizopo katika
uambishaji wa viambishi na viangami katika lugha ya Kiswahili, sheria za uundaji
wa viangami na sifa arudhi za viangami. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni
Nadharia Boreshaji ambayo iliasisiwa na Prince na Smolensky (1993). Kila sarufi
inaweza kushughulikia maumboghafi tofauti. kwa mujibu wa nadharia hii, kunafaa
kuwa na mfanano kati ya umboghafi na umbotokeo. Nadharia hii inajikita katika
sifa bia za lugha zinazotumika kuunda miundo rasmi ya lugha. Ni kwa misingi hii
ambapo utafiti huu ulijaribu kuchunguza kuwepo kwa viangami katika lugha ya
Kiswahili. Utafiti huu ulifanyiwa maktabani. Katika maktaba, mtafiti alisoma kwa
undani tafiti zilizofanywa na wanaisimu mbalimbali kuhusu viangami katika lugha
tofauti. Vitabu vingine vilivyochapishwa na vimeshughulikia viangami vilipitiwa
kwa undani. Vipengele vya utafiti vilivyohusishwa ni kama vile; mbinu za
usampulishaji, sampuli iliyotumika iliteuliwa kimakusudi. Katika uteuzi wa
sampuli, mtafiti aliteua vitabu tofauti. Mbinu za ukusanyaji wa data zilizotumiwa
ni kusoma kwa kina makala kutoka maktabani. Mtafiti aliwasilisha matokeo yake
kwa njia ya maelezo. Matokeo ya utafiti yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo na
majedwali. Kwa mujibu wa utafiti huu viangami vya Kiswahili vinaweza
kuambishwa mwanzoni na mwishoni mwa neno. Viangami vinaambishwa kwa
nomino, vitenzi, vihusishi na pia vielezi. Utafiti huu utaweza kurejelewa katika
siku za usoni kuendeleza tafiti za ziada za viangami. Utafiti huu uliazimia
kuwanufaisha wanaisimu kwani utaendeleza lugha ya Kiswahili. Wanafunzi wa
lugha ya Kiswahili na waandishi wa vitabu vitabu vya Kiswahili pia watanufaika.
Description
Tasnifu hii Inawasilishwa kKtika Idara ya Kiswahili ili Kutosheleza Baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili Katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, Mei 2021
Keywords
Uchanganuzi, Kimofosintaksia, Viangami, Lugha ya Kiswahili