Uchanganuzi wa Kimofosintaksia wa Viangami Katika Lugha ya Kiswahili

dc.contributor.advisorLeonard Chacha Mwitaen_US
dc.contributor.advisorJacktone Onyangoen_US
dc.contributor.authorNdumba, Kimonye Naomi
dc.date.accessioned2021-10-29T10:05:40Z
dc.date.available2021-10-29T10:05:40Z
dc.date.issued2021
dc.descriptionTasnifu hii Inawasilishwa kKtika Idara ya Kiswahili ili Kutosheleza Baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili Katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, Mei 2021en_US
dc.description.abstractLengo la utafiti huu ni kushughulikia uchanganuzi wa kimofosintaksia wa viangami katika lugha ya Kiswahili. Utafiti huu ulilenga kuthihirisha kuwa kuna aina tofauti za viangami katika lugha ya Kiswahili. Viangami ni mofimu zinazojisimamia kisintaksia lakini kifonolojia ni tegemezi. Viangami hutegemea neno kuu kifonolojia. Viangami huambishwa kwa neno kuu. Kiangami ni sehemu ya neno kamili inayochukua nafasi ya kiambishi. Utafiti ulilenga kuchunguza changamoto katika uainishaji wa maneno yenye viangami, tofauti zilizopo katika uambishaji wa viambishi na viangami katika lugha ya Kiswahili, sheria za uundaji wa viangami na sifa arudhi za viangami. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni Nadharia Boreshaji ambayo iliasisiwa na Prince na Smolensky (1993). Kila sarufi inaweza kushughulikia maumboghafi tofauti. kwa mujibu wa nadharia hii, kunafaa kuwa na mfanano kati ya umboghafi na umbotokeo. Nadharia hii inajikita katika sifa bia za lugha zinazotumika kuunda miundo rasmi ya lugha. Ni kwa misingi hii ambapo utafiti huu ulijaribu kuchunguza kuwepo kwa viangami katika lugha ya Kiswahili. Utafiti huu ulifanyiwa maktabani. Katika maktaba, mtafiti alisoma kwa undani tafiti zilizofanywa na wanaisimu mbalimbali kuhusu viangami katika lugha tofauti. Vitabu vingine vilivyochapishwa na vimeshughulikia viangami vilipitiwa kwa undani. Vipengele vya utafiti vilivyohusishwa ni kama vile; mbinu za usampulishaji, sampuli iliyotumika iliteuliwa kimakusudi. Katika uteuzi wa sampuli, mtafiti aliteua vitabu tofauti. Mbinu za ukusanyaji wa data zilizotumiwa ni kusoma kwa kina makala kutoka maktabani. Mtafiti aliwasilisha matokeo yake kwa njia ya maelezo. Matokeo ya utafiti yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo na majedwali. Kwa mujibu wa utafiti huu viangami vya Kiswahili vinaweza kuambishwa mwanzoni na mwishoni mwa neno. Viangami vinaambishwa kwa nomino, vitenzi, vihusishi na pia vielezi. Utafiti huu utaweza kurejelewa katika siku za usoni kuendeleza tafiti za ziada za viangami. Utafiti huu uliazimia kuwanufaisha wanaisimu kwani utaendeleza lugha ya Kiswahili. Wanafunzi wa lugha ya Kiswahili na waandishi wa vitabu vitabu vya Kiswahili pia watanufaika.en_US
dc.description.sponsorshipChuo Kikuu cha Kenyattaen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/22880
dc.language.isootheren_US
dc.publisherKenyatta Universityen_US
dc.subjectUchanganuzien_US
dc.subjectKimofosintaksiaen_US
dc.subjectViangamien_US
dc.subjectLugha ya Kiswahilien_US
dc.titleUchanganuzi wa Kimofosintaksia wa Viangami Katika Lugha ya Kiswahilien_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Uchanganuzi wa....pdf
Size:
1.09 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full text thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: