Taswira ya Malezi ya Watoto Katika Riwaya za Tumaini (2006) na Dunia Mashaka Makuu (2004)
Loading...
Date
2020-03
Authors
Mwenda, Agnes Kananu
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu unalenga kuchunguza taswira ya malezi ya watoto katika riwaya mbili za
Kiswahili ambazo ni: Tumaini ya Clara Momanyi (2006) na Dunia Mashaka Makuu ya
Lamin Omar (2004) Malezi ya watoto ni mambo halisi yanayoikumba jamii ya kisasa
ambayo inapitia mabadiliko mengi. Mabadiliko haya huwa ya kijamii, kisiasa, kiuchumi,
kidini na kiteknolojia. Waandishi wa riwaya huteua masuala yenye mguso kwa jamii na
kuyasimulia kwa kiwango cha juu cha ubunifu. Utafiti huu uliongozwa na maswali
yafuatayo: Ni mbinu zipi za malezi zinazobainika katika riwaya teule? Ni asasi na hali
gani zinazochangia katika malezi ya watoto? Mbinu za malezi zina athari gani kwa
watoto katika riwaya teule? Utafiti huu uliongozwa na malengo yafuatayo: Kueleza aina
ya malezi yanayobainika katika riwaya teule, kubainisha asasi na hali za jamii
zinazochangia katika malezi ya watoto katika riwaya teule na kueleza athari za mbinu za
malezi zinazobainika katika riwaya teule. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uhalisia
ya Gustave Flaubert (1850). Baadhi ya waitifaki wa nadharia hii ni Rene wellek (1960),
Hegel (1971) na Lukacs (1979). Nadharia ya uhalisia inaeleza kuwa kazi ya msanii
inapaswa kuwasilisha ukweli kama ulivyo katika mazingira. Baadhi ya mihimili ya
nadharia hii ni: Matukio yanayosimuliwa sharti yawe yanatokea katika ulimwengu halisi,
kazi ya msanii inapaswa kuonyesha hali ya kisaikolojia ya wahusika ambao msomaji
anakumbana nao na jinsi wanavyohisi na kutenda wanapokumbana na hali Fulani na
wahusika huwa halisi na lugha wanayotumia huwa rahisi. Huku mtafiti akiongozwa na
mihimili ya nadharia alihakiki riwaya zilizoteuliwa ili kupata data iliyotoshelesha
mahitaji ya utafiti huu. Uteuzi wa sampuli ulitumika na riwaya mbili ziliteuliwa: Tumaini
ya Clara Momanyi (2006) na Dunia Mashaka Makuu ya Lamin Omar (2004). Riwaya
hizi zilitupa data faafu katika utafiti huu. Utafiti huu ulifanywa maktabani. Mtafiti
alisoma kwa kina vitabu vya fasihi, majarida na tasnifu zilizoandikwa awali ili
kufanikisha kazi yake. Data iliyopatikana ilichanganuliwa kulingana na malengo na
maswali ya utafiti pamoja na mihimili ya nadharia. Data iliwasilishwa kwa maelezo
katika sura tano. Utafiti huu umekusudiwa kuwafaa wanafunzi, walimu, wahakiki na
waandishi wengine katika kubainisha umuhimu wa kuwapa watoto malezi mema. Pia,
utawafaidi walezi na jamii kwa jumla.
Description
Tasnifu hii Imewasilishwa Katika Idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika ya Chuo Kikuu cha Kenyatta ili
Kutoshelesha Baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili. Machi, 2020
Keywords
Taswira, Malezi ya Watoto, Riwaya za Tumaini (2006), Dunia Mashaka Makuu (2004)