• English
    • français
  • English 
    • English
    • français
  • Login
View Item 
  •   Repository Home
  • Master Theses and Dissertations(MST)
  • MST-School of Humanities and Social Sciences
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • View Item
  •   Repository Home
  • Master Theses and Dissertations(MST)
  • MST-School of Humanities and Social Sciences
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • View Item
JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

Dhima ya lugha teule katika kuwasilisha taswira ya mtoto katika jamii ya abagusii tasnifu

Thumbnail
View/Open
Full text thesis (930.9Kb)
Date
2018
Author
Ombaye, Robert Omuga
Metadata
Show full item record
Abstract
Utafiti huu ulichunguza dhima ya lugha teule katika kuwasilisha taswira ya mtoto katika jamii ya Abagusii. Malengo ya utafiti huu yalikuwa kutambua lugha iliyowasilisha taswira ya mtoto na kubainisha dhima na athari zake katika jamii ya Abagusii. Nadharia ya Ethnografia ya Mawasiliano iliyoasisiwa na Hymes (1964) ilitumika katika utafiti huu. Nadharia hiyo ilifaa kwa sababu iliangazia jinsi mawasiliano yalivyochanganuliwa kwa kuzingatia vipengele vya: mada, umbo la ujumbe, muktadha, wahusika, sababu za mawasiliano, kanuni za ufafanuzi wa ujumbe, njia za mawasiliano na utendaji. Data ya kimsingi ilipatikana kutoka eneo bunge la Nyaribari Chache, Ugatuzi Mdogo wa Kisii ya Kati, Kaunti ya Kisii. Aidha, data nyingine ilikusanywa maktabani kwa kusoma vitabu, kumbukumbu, ripoti, tasnifu, makala na majalida kuhusu mada ya utafiti. Nyanjani mtafiti alitumia sampuli iliyoteuliwa kwa kutumia mbinu ya kimakusudi kuwahoji watu sabini na wawili. Mbinu ya makusudi ilitumiwa kupata watafitiwa walioimudu vyema lugha ya Ekegusii kuhojiwa ili kupata matokeo faafu. Mtafiti aliwahoji watu wawili (2) kutoka kila kikundi; watoto, vijana, watu wazima, naibu wa machifu, machifu na wataalamu wa haki za watoto kutoka wodi sita (6) za eneo bunge la Nyaribari Chache. Vifaa vilivyotumiwa kuwahoji ni hojaji wazi na maswali ya mahojiano ya ana kwa ana na wahojiwa. Data iliyokusanywa ilirekodiwa na kuchanganuliwa kwa kuzingatia maswali, malengo na nadharia ya utafiti. Matokeo ya utafiti huu yaliwasilishwa kwa kutumia maelezo na yalibainisha kuwa, lugha hasi na chanya ilitumika katika kuwasilisha taswira mbalimbali za watoto katika jamii ya Abagusii. Matokeo ya utafiti huu vilevile yalibainisha kuwa dhima za lugha hiyo ni: kuelimisha, kukuza maadili, kuonya, kurekebisha tabia, kuwasiliana, kutia motisha, kusifu, kufariji, kulinganisha, kushauri na kukemea. Aidha, matokeo ya utafiti huu yalibainisha kuwa lugha hiyo ilizua athari kadhaa kwa mtoto ambazo ni: kuhama kutoka nyumbani kwao, kutelekezwa, kubaguliwa, kukata tamaa, kuchanganyikiwa akili, kuwa na tabia nzuri au mbaya, kupendwa, kukubalika na kufurahi. Utafiti huu ulikuwa wa manufaa katika jamii ya Abagusii kwa vile uliwawezesha kuelewa kuhusu lugha iliyowasilisha taswira ya mtoto. Ufahamu wa lugha hiyo ni muhimu kwa vile ulichangia katika kuamua maisha ya mtoto siku za usoni. Aidha, ufahamu huo ulichangia pakubwa katika utoaji wa mielekeo, maoni na matendo ya watu wazima kwa watoto katika jamii ya Abagusii.
URI
http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/18557
Collections
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages [234]

Designed by Library ICT Team copyright © 2017 
Contact Us | Send Feedback

 

 

Browse

All of RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

My Account

LoginRegister

Designed by Library ICT Team copyright © 2017 
Contact Us | Send Feedback