Usasa katika Ngoma ya Itheke.
Abstract
Malengo ya utafiti huu yalikuwa ni kutathmini usasa katika ngoma ya Itheke. Utafiti ulifanywa ili kubainisha jinsi usasa unavyoisaidia ngoma ya Itheke kuimarika na kuwa maarufu miongoni mwa j imii ya Wakamba. Aidha utafiti ulidhamiria kubainisha jinsi usasa unavyoiwezesha ngoma ya Itheke kutekeleza majukumu ya kijamii.
Nadharia za usasa na uamali zimetumiwa kwa pamoja katika utafiti huu. Nadharia ya usasa imetuongoza kubainisha jinsi usasa unavyodhihirika katika vipengele vya ngoma ya Itheke ambavyo ni: lugha na mtindo, maudhui, muktadha, teknolj is ya kisasa, hadhira , ala na maleba. Nadharia ya uamali hasa kipengele cha Ethnografia ya mazungumzo kilitumika kubainisha jinsi vipengele vya ngoma ya Itheke vinavyotekeleza majukumu ya kijamii miongoni mwa jamii ya Wakamba.
Ili kubainisha jinsi jamii ya Wakamba imekuwa ikikua na kubadilika, historia ya chimbuko la jamii Wakamba imedokezwa. Mabadiliko yalionekana kuadhiri mifumo yote ya kimaisha ikiwa ni pamoja na fasihi simulizi ya jamii ya Wakamba.
Kwa sababu ya mabadiliko ya maisha, ngoma nyingi katika jamii ya Wakamba zimedidimia huku zingine zikiibuka. Ngoma ya Itheke ni mojawapo ya ngoma zilizoibuka na kuwa maarufu kwa sababu ya usasa. Utafiti huu umeonyesha sababu za ngoma ya Itheke kuwa maarufu wakati ngoma zingine zinapodidimia na kusahaulika.