Tamthilia kama utendi:uchanganuzi linganishi wa tamthilia za Kinjeketile na mzalendo Kimathi

Loading...
Thumbnail Image
Date
2011-11-02
Authors
Ireri, Kahara J.
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafti huu umechunguza tamthilia ya Kiswahili kama utendi. Uchunguzi umejikita katika tamthilia mbili za Kiswahili; Kinjeketile (1969) na Mzalendo Kimathi (1975). Malengo ya tasnifu hii yalikuwa kuchunguza jinsi utendi unavyotumika kuchanganulia tamthilia ya Kiswahili. Aidha kudhihirisha jinsi utendi unavyotumiwa kusawiri wahusika, ujumbe na lugha. Hatimaye kuonyesha kwamba watunzi wa tamthilia wanatumia utendi kama mtindo. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni ile ya mwingilianomatini ambayo ni mkabala wa kuelezea maana za matini kwa kurejelea matini zingine. Nadharia hii ina asili yake katika isimu ya karne ya 20, hasa katika kazi ya mwanaisimu wa Kiswisi, Ferdinand de Saussure. Kwake de Saussure, ishara za kiisimu hupata maana kwa sababu ya uhusiano wa kishirika na kimuungano na ishara zingine za kiisimu. Mtazamo wa Bakhtin pia una mchango mkubwa sana kwa nadharia hii. Kwake Bakhtin, maneno huishi katika maeneo fulani ya kijamii, sajili fulani za kijamii na kitambo cha matamko na kupokelewa kwa matamko hayo. Sura ya kwanza ambayo ni utangulizi imeshughulikia suala la utafiti, sababu za kuchagua mada, upeo wa utafiti, madhumuni ya utafiti, msingi wa nadharia, yalioandikwa kuhusu mada na mbinu za utafiti. Sura ya pili imeshughulikia historia ya tamthilia ya Kiswahili na maendeleo yake, pamoja na dhana ya utendi na ubia wake. Sura ya tatu imejadili matumizi ya utendi katika usawiri wa wahusika. Katika sura ya nne, mtafiti amechunguza umuhimu wa utendi katika usawiri wa ujumbe na lugha. Sura ya tano ni hitimisho. Mtafiti ametoa muhtasari, matokeo kuhusu utafiti na mapendekezo.
Description
Department of Kiswahili,146p.The PL 8704 .K3T3 2011
Keywords
Citation