Tamthilia kama utendi:uchanganuzi linganishi wa tamthilia za Kinjeketile na mzalendo Kimathi

dc.contributor.authorIreri, Kahara J.
dc.date.accessioned2011-11-02T09:07:41Z
dc.date.available2011-11-02T09:07:41Z
dc.date.issued2011-11-02
dc.descriptionDepartment of Kiswahili,146p.The PL 8704 .K3T3 2011
dc.description.abstractUtafti huu umechunguza tamthilia ya Kiswahili kama utendi. Uchunguzi umejikita katika tamthilia mbili za Kiswahili; Kinjeketile (1969) na Mzalendo Kimathi (1975). Malengo ya tasnifu hii yalikuwa kuchunguza jinsi utendi unavyotumika kuchanganulia tamthilia ya Kiswahili. Aidha kudhihirisha jinsi utendi unavyotumiwa kusawiri wahusika, ujumbe na lugha. Hatimaye kuonyesha kwamba watunzi wa tamthilia wanatumia utendi kama mtindo. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni ile ya mwingilianomatini ambayo ni mkabala wa kuelezea maana za matini kwa kurejelea matini zingine. Nadharia hii ina asili yake katika isimu ya karne ya 20, hasa katika kazi ya mwanaisimu wa Kiswisi, Ferdinand de Saussure. Kwake de Saussure, ishara za kiisimu hupata maana kwa sababu ya uhusiano wa kishirika na kimuungano na ishara zingine za kiisimu. Mtazamo wa Bakhtin pia una mchango mkubwa sana kwa nadharia hii. Kwake Bakhtin, maneno huishi katika maeneo fulani ya kijamii, sajili fulani za kijamii na kitambo cha matamko na kupokelewa kwa matamko hayo. Sura ya kwanza ambayo ni utangulizi imeshughulikia suala la utafiti, sababu za kuchagua mada, upeo wa utafiti, madhumuni ya utafiti, msingi wa nadharia, yalioandikwa kuhusu mada na mbinu za utafiti. Sura ya pili imeshughulikia historia ya tamthilia ya Kiswahili na maendeleo yake, pamoja na dhana ya utendi na ubia wake. Sura ya tatu imejadili matumizi ya utendi katika usawiri wa wahusika. Katika sura ya nne, mtafiti amechunguza umuhimu wa utendi katika usawiri wa ujumbe na lugha. Sura ya tano ni hitimisho. Mtafiti ametoa muhtasari, matokeo kuhusu utafiti na mapendekezo.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/1533
dc.language.isootheren_US
dc.titleTamthilia kama utendi:uchanganuzi linganishi wa tamthilia za Kinjeketile na mzalendo Kimathien_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Tamthilia kama utendi uchanganuzi linganishi.....pdf
Size:
67.11 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
full text thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: