Makosa ya Kisintaksia Katika Uandishi wa Insha za Kiswahili za Wanafunzi wa Shule za Upili.
Loading...
Date
2012
Authors
Gathunga, John Kariuki.
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu ulitekelezwa kwa madhumuni ya kuchanganua na kujadili makosa ya
kisintaksia katika insha za wanafunzi wa shule za upili. Kusudi la kuchanganua makosa
lilikuwa kubainisha chanzo cha makosa husika kwa madhumuni ya kupendekeza mbinu
mwafaka za kutumiwa na walimu ili ufunzaji wa insha uimarike. Swala la utafiti
lilitegemea usugu wa makosa mahsusi ya kisintaksia katika insha za wanafunzi wa shule
za upili. Uchanganuzi ulitumikiza mihimili ya kanuni za Nadharia ya Sintaksia Finyizi
hasa kanuni ya ufungami. utegernezi muundo, ufasiri karnili, leksia na uarifu. adharia
ya Sintaksia Finyizi ilitekelezwa katika muktadha wa falsafa pana ya Sarufi Bia ya
Chomsky (Cook na ewson 1996). Swala la utafiti lilikuwa kudhihirisha makosa
mahsusi ya kisintaksia katika insha za wanafunzi wa shule za upili. Mbinu za utafiti
zilijumuisha nyanjani na maktabani. Matokeo ya utafiti yaliwakilishwa kwa njia ya
maelezo katika sura tano.
Sura ya kwanza ilichambua usuli wa mada, ikabainisha swala la utafiti, maswali na
malengo ya utafiti, misingi ya kuchagua mada, upeo wa utafiti, tahakiki ya maandishi,
misingi ya kinadharia na mbinu za utafiti. Sura ya pili ilifafanua muundo wa sentensi ya
Kiswahili ili kutambulisha na kuchanganua kategoria leksia na amilifu, virai leksia na
amilifu, na muungano wa virai katika kuunda sentensi sahihi. Sura ya tatu ilifululiza
uchanganuzi wa aina na usugu wa makosa. Sura ya nne ilijadili chanzo cha makosa
husika kabla ya kuuhitimisha utafiti katika sura ya tano. Mahitimisho yalidhihirisha kuwa
makosa ya kisintaksia yalijitokeza katika vitengo vyote vitano vilivyotumikizwa.
Description
Tasnifu Iliyoandikwa kwa Madhumuni ya Kutosheleza Baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili wa Chuo Kikuu cha Kenyatta, 2012.