Makosa ya Kisintaksia Katika Uandishi wa Insha za Kiswahili za Wanafunzi wa Shule za Upili.

dc.contributor.advisorKing'ei, Kitula Osore, Miriam
dc.contributor.authorGathunga, John Kariuki.
dc.date.accessioned2016-11-23T12:38:07Z
dc.date.available2016-11-23T12:38:07Z
dc.date.issued2012
dc.descriptionTasnifu Iliyoandikwa kwa Madhumuni ya Kutosheleza Baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili wa Chuo Kikuu cha Kenyatta, 2012.en_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulitekelezwa kwa madhumuni ya kuchanganua na kujadili makosa ya kisintaksia katika insha za wanafunzi wa shule za upili. Kusudi la kuchanganua makosa lilikuwa kubainisha chanzo cha makosa husika kwa madhumuni ya kupendekeza mbinu mwafaka za kutumiwa na walimu ili ufunzaji wa insha uimarike. Swala la utafiti lilitegemea usugu wa makosa mahsusi ya kisintaksia katika insha za wanafunzi wa shule za upili. Uchanganuzi ulitumikiza mihimili ya kanuni za Nadharia ya Sintaksia Finyizi hasa kanuni ya ufungami. utegernezi muundo, ufasiri karnili, leksia na uarifu. adharia ya Sintaksia Finyizi ilitekelezwa katika muktadha wa falsafa pana ya Sarufi Bia ya Chomsky (Cook na ewson 1996). Swala la utafiti lilikuwa kudhihirisha makosa mahsusi ya kisintaksia katika insha za wanafunzi wa shule za upili. Mbinu za utafiti zilijumuisha nyanjani na maktabani. Matokeo ya utafiti yaliwakilishwa kwa njia ya maelezo katika sura tano. Sura ya kwanza ilichambua usuli wa mada, ikabainisha swala la utafiti, maswali na malengo ya utafiti, misingi ya kuchagua mada, upeo wa utafiti, tahakiki ya maandishi, misingi ya kinadharia na mbinu za utafiti. Sura ya pili ilifafanua muundo wa sentensi ya Kiswahili ili kutambulisha na kuchanganua kategoria leksia na amilifu, virai leksia na amilifu, na muungano wa virai katika kuunda sentensi sahihi. Sura ya tatu ilifululiza uchanganuzi wa aina na usugu wa makosa. Sura ya nne ilijadili chanzo cha makosa husika kabla ya kuuhitimisha utafiti katika sura ya tano. Mahitimisho yalidhihirisha kuwa makosa ya kisintaksia yalijitokeza katika vitengo vyote vitano vilivyotumikizwa.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/15174
dc.language.isoenen_US
dc.publisherKenyatta Universityen_US
dc.titleMakosa ya Kisintaksia Katika Uandishi wa Insha za Kiswahili za Wanafunzi wa Shule za Upili.en_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Makosa ya kisintaksia......pdf
Size:
61.15 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full Text Thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: