RP-Department of Kiswahili and African Languages
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing RP-Department of Kiswahili and African Languages by Subject "Babu Alipofufuka"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Mbinu Ya Ubunilizi wa Kisayansi Katika Riwaya: Bina-Adamu (K. W. Wamitila) na Babu Alipofufuka (S. A. Mohamed)(International Academic Journal of Social Sciences and Education (IAJSSE), 2018-11) Mucee, Franklin Mukembu; Wafula, Richard Makhanu; King’ei, G. K.Utafiti huu ulihusu mbinu ya Ubunilizi wa Kisayansi katika mtindo wa riwaya teule za Bina Adamu K. W. Wamitila (2002) na ile ya Babu Alipofufuka ya S.A. Mohamed (2001). Utafiti huu hivyo basi umeonyesha kwamba sayansi bunilizi ni kipera cha riwaya kinachopatikana katika fasihi ya Kiswahili na ambacho kinaendeleza maudhui ya sayansi na teknolojia katika utamaduni wa jamii zinazotumia lugha ya Kiswahili kuwasiliana. Malengo ya utafiti huu yalijikita katika kubainisha maana ya sayansi bunilizi na. kudhihirisha sifa za sayansi bunilizi zinazopatikana katika riwaya hizi. Vile vile utafiti huu ulilenga kudhihirisha-kwamba riwaya hizi zinashughulikia sayansi bunilizi mbali na kuonyesha mbinu za kimasimulizi zinazozifanya riwaya za Babu Alipofufuka na Bina-Adamu kuwa sayansi bunilizi. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya sayansi bunilizi ambayo imehusishwa na mawazo yake Jules Verne na H.G. Wells (1950), nadharia inayoshikilia maudhui ya sayansi na teknolojia ya wakati uliopo na wakati ujao, mtindo wa kinjozi ambapo matukio ya kiajabu yanahusishwa na usimulizi usioaminika katika misingi ya uhalisia. Nadharia hii pia haionyeshi mahali na nyakati, zinaweza kuwa ni zijazo. Aidha hushughulikia maswala ya athari za sayansi na teknolojia dhidi ya maadili ya jamii. IIi kufanikisha utafiti huu data yote iliyohitajika ilikusanywa kutoka maktabani ambapo maktaba nyingi zilitembelewa kwa lengo la kukusanya data iliyohusiana na yale yaliyoandikwa kuhusu mada ya utafiti. Mtafiti alidurusu yaliyoandikwa kuhusu sayansi bunilizi katika riwaya teule. Majarida, majuzuu, tasnifu na machapisho mengine yanayohusiana na kuafiki mada na malengo ya utafiti yalipekuliwa. Riwaya teule ambazo ni Bina-Adamu (2002) na Babu Alipofufuka (2001) zilisomwa na kuchambuliwa kwa kina ili kubainisha malengo ya utafiti yanayozifanya riwaya hizi kuwa sayansi bunilizi. Data iliyopatikana kwenye riwaya hizi ilichanganuliwa kwa kunukuliwa kwenye daftari kwa kuzingatia malengo ya utafiti kisha baadaye data hii ikawasilishwa kwa njia ya mae1ezo yaliyozingatia ufafanuzi wa sayansi bunilizi kama kipera cha fasihi ya Kiswahili katika riwaya. Uwasilishaji wa data ulijifunga katika malengo ya utafiti pamoja na mihimili ya nadharia teule ya sayansi bunilizi. Utafiti huu umekuwa na mchango mkubwa kwa kuwa mada ya sayansi bunilizi katika fasihi ya Kiswahili imebainisha uwiano kati ya maendeleo ya sayansi na teknolojia na sayansi bunilizi ya Kiswahili katika eneo la Afrika Mashariki. Kwa kuwa sayansi bunilizi huzungumzia mambo ya kiajabu na mapya, imeweza kuzua msamiati mpya ambao utaingizwa katika lugha ya Kiswahili na hivyo kupanua msamiati wa lugha ya Kiswahili kwa jumla. Huu ni mchango chanya kwani lugha ya Kiswahili ingali inakua.