RP-Department of Kiswahili and African Languages
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing RP-Department of Kiswahili and African Languages by Subject "Asasi ya Familia"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Uhusiano kati ya Asasi ya Familia na Uongozi wa Jamii katika Riwaya za Kiswahili Dunia Yao (Mohamed 2006) na Kidagaa Kimemwozea (Walibora 2012)(Eastern Africa Journal of Contemporary Research (EAJCR), 2019) Muusya, Justus Kyalo; King’ei, Kitula; Wafula, Richard M.Asasi ya familia ndio msingi wa kila jamii. Uongozi wa familia kwa hivyo huweza kupiga mwangwi uongozi wa jamii nzima. Huku ni kusema kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya namna familia zinavyoongozwa na uongozi wa jamii pana. Inakisiwa kuwa viongozi wengi wa jamii huwa na familia. Hii ina maana kuwa iwapo viongozi hawa wataweza kuongoza familia zao vyema kwa kuzingatia amali na maadili yatakiwayo, basi suala hili litajitokeza katika kiwango cha kitaifa. Na ikiwa viongozi watapotoka kimaadili katika kuzielekeza familia zao, basi upotovu huu utajitokeza katika uongozi wao wa jamii katika kiwango kingine. Makala haya yanalenga kuchunguza ikiwa katika riwaya za Kiswahili kuna uhusiano katika namna ambavyo familia zinaongozwa kwa upande mmoja na uongozi wa jamii kitaifa kwa upande mwingine. Utafiti awali unaonyesha kuwa kiongozi anayeshindwa kukuza na kuongoza familia yake ipasavyo huweza kushindwa vilevile kuongoza jamii katika ngazi za juu. Inakisiwa kuwa hii ni kwa sababu kiongozi huyo huwa amepotoka kimaadili. Kwa misingi hii, kiongozi ambaye anazingatia maadili bora, maadili hayo yataweza kujitokeza katika kiwango cha kifamilia sawa na kiwango cha kitaifa. Je, tunaweza kukisia mienendo ya kiongozi wa dola kwa kutathmini namna anavyoongoza familia yake? Je, tunaweza kubashiri uongozi wa familia ya kiongozi kwa kutathimini matendo yake katika ngazi ya kitaifa? Haya ni baadhi ya maswali ambayo tumeyajibu katika uchunguzi huu. Kwa hivyo, lengo la makala haya ni kuchunguza ikiwa makisio haya ni kweli au si kweli. Data ya utafiti huu ilikusanywa katika riwaya mbili zilizoteuliwa katika uchunguzi huu. Hizi ni Dunia Yao (Mohamed 2006) na Kidagaa Kimemwozea (Walibora 2012). Uchunguzi huu uliongozwa na nadharia ya daindamano. Hii ni nadharia ya kutathmini maadili ya viongozi katika jamii.