Browsing by Author "Kinara, Gladys"
Now showing 1 - 3 of 3
Results Per Page
Sort Options
Item Individual Alienation and Political Oppression in Kenya as Depicted in Wahome Mutahi’s Novels(Scholarlink Research Institute Journals, 2012) Kinara, GladysThe study was an attempt to analyze how Wahome Mutahi, in a selected three of his texts, engages the political concerns of his time in Kenya. Though there is no mention of Kenya, the events featured obtained in Kenya in the writer’s time. Similarly, some characters in the fiction are patterned after historical characters in Kenya at the period mediated in the works. Primary data was obtained from a critical reading of Wahome Mutahi’s selected novels, namely Three Days on the Cross (1991), The Jail Bugs (1992) and Doomsday (1999). Other materials, especially Wahome Mutahi’s `Whispers’ column in the Sunday Nation, formed the secondary sources, and relevant critical works were read and cited to support the study. The texts present a universe fragmented by political misrule, which induces alienation to individual characters. The worlds evoked in these works are characterized by political oppression and the major characters in the works are alienated. Chipota and Momodu in Three Days on the Cross, Albert Kweyu in The Jail Bugs and Ismail and Albert Lukulo in Doomsday are all alienated characters living in societies where political oppression obtains. The study is a useful addition to the corpus of emergent research into and knowledge about the significance of this previously neglected Kenyan writer, dramatist and journalist, Wahome Mutahi.Item Mapokeo na upya katika utenzi wa mwana kupona na vimelea vyake(Kenyatta University, 2025-10) Kinara, GladysUtafiti huu ulichunguza mapokeo na upya katika Utenzi wa Mwana Kupona na vimelea vyake. Utafiti huu ulichochewa na hoja kuwa Utenzi wa Mwana Kupona ni maarufu na umeshughulikiwa na wataalam mbalimbali kufikia sasa. Hata hivyo, tangu utenzi huo kutungwa mwaka wa 1858 kumekuwa na washairi mbalimbali ambao wametunga tenzi zinazoelekea kuwa mwangwi wa utenzi huo na yaelekea kuwa utafiti wa aina hiyo haujatiliwa maanani. Ili kuziba pengo hilo, uchanganuzi ulifanywa kwa kuzingatia tungo zikiwemo Utenzi wa Mwana Kupona uliotungwa 1858 na kuchapishwa 1971 na Allen, J. W. T., ‘Utenzi wa Hati’ na ‘Utenzi wa Adili’ katika tawasifu ya Shaaban Robert ya; Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini (1967). Utenzi wa Howani Mwana Howani uliotungwa na Zaynab Himid Mohammed mwaka wa 1983 na utenzi wa Jawabu la Mwana Kupona uliotungwa na EL-Maawy mwaka wa 2011. Utafiti huu ulilenga kuchunguza vipengele vya mapokeo katika Utenzi wa Mwana Kupona, kubainisha muumano katika Utenzi wa Mwana Kupona na vimelea vyake na kujadili upya katika vimelea vya Utenzi wa Mwana Kupona. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Ki-Bakhtin kuhusu lugha. Nadharia hii ilibuniwa na Mikhail Bakhtin na kuendelezwa na Clark na Holquist (1984), Farmer (1998), Hirschkop (2001), Holquist (2002), Brandist (2002) kati ya wengine. Kwa mujibu wa nadharia hii, lugha au usemi wowote una nguvu za aina mbili: nguvu za kani kitovu na nguvu za kani pewa. Nguvu za kani kitovu ni sehemu ya lugha inayoelekezwa kwenye kitovu au katika mhimili mkuu wa mzunguko. Nguvu za kani pewa nazo ni sehemu ya lugha inayovuta kwenda nje ya kitovu. Nguvu kati ya kani kitovu na kani pewa ziliwasilisha mabadiliko ya lugha na zilihakikisha kuwa daima mabadiliko hayo yalibakia kushindana. Mhimili wa kani kitovu ulitumiwa kuchunguza mapokeo katika Utenzi wa Mwana Kuponana muumano uliopo kati ya Utenzi wa Mwana Kupona na vimelea vyake. Nao mhimili wa kani pewa ulitumiwa kuchunguza upya katika vimelea vya Utenzi wa Mwana Kupona. Utafiti huu ulikuwa wa kimaelezo. Utafiti ulijikita maktabani na nyanjani. Mtafiti alizuru maktaba mbalimbali zikiwemo za vyuo, kitaifa na dafina mbalimbali kama Research Institute of Swahili Studies of Eastern Africa (RISSEA) kwa lengo la kupata data faafu ya utafiti huu. Maktabani, vitabu, makala, majarida na wavuti zilisomwa kwa kina ili kupata data iliyosaidia katika kuweka msingi wa utafiti huu. Nyanjani, mtafiti alizuru eneo la Lamu kwa lengo la kupata mawazo ya wahojiwa kuhusu Utenzi wa Mwana Kupona. Mawazo hayo yalitumiwa kushadidia utafiti husika. Mtafiti alitumia maswali ya mwongozo wa mahojiano na mjadala ili kupata maoni ya wahojiwa yaliyochangia ufanisi wa utafiti huu. Sampuli iliteuliwa kimaksudi. Vitabu vilisomwa kwa kina ili kupata data faafu ya utafiti huu. Uchanganuzi ulifanywa kwa kuzingatia mihimili ya nadharia ya ki-Bakhtin kuhusu lugha pamoja na malengo ya utafiti. Data iliwasilishwa kwa njia ya maelezo katika sura mbalimbali. Ilibainika kwamba; tenzi hizi kwa kiasi kikubwa ziliazima kutoka katika Utenzi wa Mwana Kupona kifani na kimaudhui. Mambo waliyoazima yalikuwa mapokeo ambayo yalirithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Hata hivyo, japo warithi wa Mwana Kupona waliazima kutoka katika Utenzi wa Mwana Kupona, waliongeza upya katika tenzi zao ili kukidhi mahitaji ya wakati wao na hivyo kuzifanya tenzi hizi kuwa mwangwi wa Utenzi wa Mwana Kupona. Utafiti huu utachangia wasomi wa masuala ya fasihi ya Kiswahili katika kuonyesha uwezo wa vimelea vya Utenzi wa Mwana Kupona kama vifaa muhimu katika kuangazia mageuzi yaliyotokea katika jamii katika mpito wa wakatiItem Maudhui ya ukimwi katika ua la faraja na kala tufaha(2012-07-05) Kinara, Gladys; Masinde, E. W.; Pamela NgugiUtafiti huu umechunguza jinsi riwaya za: Ua la Faraja (2005) na Kala Tufaha (2007) zilivyosawiri usemi unaokusudia kuwapa tumaini walioathiriwa na maradhi ya UKIMWI na kuonya wasio na maradhi haya dhidi ya mienendo inayoweza kuwafanya kuambukizwa. Katika kuchunguza jinsi riwaya hizi zilivyosawiri suala la UKIMWI, utafiti huu umechunguza usemi unaotumiwa kuusawiri UKIMWI, athari ya maradhi haya kwa wahusika katika riwaya husika, na kuonyesha nafasi ya riwaya hizi katika kukabiliana na suala zima la UKIMWI pamoja na changamoto zinazotokea. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Naratolojia pamoja na ya Matendo ya Usemi. Kwa kuongozwa na mihimili ya nadharia zilizotumiwa, mtafiti alihakiki riwaya zilizoteuliwa ili kupata data iliyotosheleza mahitaji ya utafiti. Data iliyopatikana imerekodiwa na kuchanganuiiwa kulingana na malengo na maswali ya utafiti pamoja na mihimili ya nadharia. Data imewasilishwa kwa maelezo katika utaratibu huu: Sura ya kwanza ya utafiti imetanguliza mada, maswali yanayoongoza utafiti, malengo ya utafiti, upeo na mipaka, yaliyoandikwa kuhusu mada, sababu ya kuchagua mada na misingi ya nadharia. Sura ya pili imechunguza usemi uliotumiwa kusawiri UKIMWI katika riwaya husika. Sura ya tatu imechunguza athari ya maradhi ya UKIMWI kwa wahusika. Sura ya nne imechunguza nafasi ya masimulizi haya katika kukabiliana na suala la UKIMWI na changamoto zake. Utafiti huu pia umedengua maana zilizohusishwa na maradhi ya UKIMWI na kuwapa matumaini wanaougua na walioathiriwa. Tumehitimisha utafiti wetu na kutoa mapendekezo kwa tafiti zijazo katika sura ya tano. Utafiti huu umekusudiwa kuwafaa wasomi, watafiti, taaluma ya udaktari, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayoshughulika na kukabiliana na suala la UKIMWI na wanajamii kwa jumla.