Maudhui ya ukimwi katika ua la faraja na kala tufaha

Loading...
Thumbnail Image
Date
2012-07-05
Authors
Kinara, Gladys
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu umechunguza jinsi riwaya za: Ua la Faraja (2005) na Kala Tufaha (2007) zilivyosawiri usemi unaokusudia kuwapa tumaini walioathiriwa na maradhi ya UKIMWI na kuonya wasio na maradhi haya dhidi ya mienendo inayoweza kuwafanya kuambukizwa. Katika kuchunguza jinsi riwaya hizi zilivyosawiri suala la UKIMWI, utafiti huu umechunguza usemi unaotumiwa kuusawiri UKIMWI, athari ya maradhi haya kwa wahusika katika riwaya husika, na kuonyesha nafasi ya riwaya hizi katika kukabiliana na suala zima la UKIMWI pamoja na changamoto zinazotokea. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Naratolojia pamoja na ya Matendo ya Usemi. Kwa kuongozwa na mihimili ya nadharia zilizotumiwa, mtafiti alihakiki riwaya zilizoteuliwa ili kupata data iliyotosheleza mahitaji ya utafiti. Data iliyopatikana imerekodiwa na kuchanganuiiwa kulingana na malengo na maswali ya utafiti pamoja na mihimili ya nadharia. Data imewasilishwa kwa maelezo katika utaratibu huu: Sura ya kwanza ya utafiti imetanguliza mada, maswali yanayoongoza utafiti, malengo ya utafiti, upeo na mipaka, yaliyoandikwa kuhusu mada, sababu ya kuchagua mada na misingi ya nadharia. Sura ya pili imechunguza usemi uliotumiwa kusawiri UKIMWI katika riwaya husika. Sura ya tatu imechunguza athari ya maradhi ya UKIMWI kwa wahusika. Sura ya nne imechunguza nafasi ya masimulizi haya katika kukabiliana na suala la UKIMWI na changamoto zake. Utafiti huu pia umedengua maana zilizohusishwa na maradhi ya UKIMWI na kuwapa matumaini wanaougua na walioathiriwa. Tumehitimisha utafiti wetu na kutoa mapendekezo kwa tafiti zijazo katika sura ya tano. Utafiti huu umekusudiwa kuwafaa wasomi, watafiti, taaluma ya udaktari, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayoshughulika na kukabiliana na suala la UKIMWI na wanajamii kwa jumla.
Description
Department of Kiswahili and African Languages: 135p. The PL 8704 .K5M32 2012
Keywords
Mkufya, W. E. Ua la faraja, History and criticism, Babu Omar, Kala tufaha, AIDS (Disease), Kenya, HIV infections
Citation